Friday 29th, March 2024
@Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl. J.K Nyerere (SabaSaba) Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam
Maonesho ya biashara yanayojulikana kama sabasaba yalianza mwaka 1962 yakiwa ni maonesho ya Kilimo yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya Wizara ya Biashara na Ushirika.Maonesho hayo yalikuwa na lengo la kukuza kilimo na ushirika.
Mwaka 1978 serikali iliunda Bodi ya Biashara ya nje kupitia sheria yake namba 5 ya mwaka huo, Bodi hiyo ilipewa mamlaka kushughulikia usafirishaji wa bidhaa za kitanzania nje ya nchi. Bodi ya Biashara ya nje ilipewa pia dhamana ya kukuza ushirikiano wa biashara ya kimataifa kupitia maonesho ya kibiashara, kufanya utafiti kuhusiana na biashara.
Miaka ya hivi karibuni maonesho hayo yamekuwa yakishirikisha nchi takribani 20 kutoka kusini mwa Afrika (SADC) vilevile yamejulikana kama maonesho ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam na viwanja vinajulikana kama viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Nyerere.
Kauli mbiu ya mwaka 2018 ni: "Ukuzaji wa Biashara kwa Maendeleo ya Viwanda"
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.