• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Rasimali watu na Utawala
      • Idara ya fedha na Biashara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Mipango,Sera na Takwimu
      • Ardhi na Maliasilli
      • Maji
      • Ujenzi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Mazingira na Usafi
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Mipango na Uongozi
      • Elimu, Afya na Maji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Ardhi
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi Au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Historia

TAARIFA FUPI YA WILAYA (DISTRICT PROFILE)

 

1.1       MAHALI ILIPO

Wilaya ya Mkuranga ni mojawapo kati ya Wilaya 9 za Mkoa wa Pwani.  Ipo katikati ya latitude 6o.35 o na 7o.15o Kusini mwa Ikweta; na Longitudi 38o.15o na 39o.30o Mashariki mwa Meridian. Wilaya ya Mkuranga inapakana na Wilaya ya Temeke kwa upande wa Kaskazini, Ilala upande wa Kaskazini Magharibi kwa upande wa Kusini inapakana na WIlaya ya Wilaya ya Kibiti, Upande wa Mashariki inapakana na Bahari ya Hindi na upande wa Magharibi inapakana na Wilaya ya Kisarawe. Wilaya ya Mkuranga ina ukubwa wa eneo la Km. za mraba 2,432 kati ya hizo Km. za mraba 447 ni za maji (Bahari ya Hindi) na Km. za mraba 1985 za nchi kavu ambapo eneo la km. za mraba 1934 linafaa kwa kilimo.

HALI YA HEWA NA SURA YA NCHI

Wilaya ya Mkuranga ipo katika ukanda wa mashariki mwa Pwani ya Bahari ya Hindi.  Hali ya hewa ni ya kuridhisha, Wilaya hupata mvua katika vipindi 2 kwa mwaka.  Kipindi cha Novemba hadi Desemba (Vuli) na kipindi cha mwezi Machi hadi Juni (Mvua za Masika).  Kwa wastani Wilaya hupata mvua kati ya mm.800 hadi mm.1,000 kwa mwaka na wastani wa nyuzijoto 28o.

IDADI YA WATU

Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya Taifa ya mwaka 2012, wakazi wa Wilaya ya Mkuranga ni 222,921 wakiwemo wanawake 108,024 na wanaume 114,897.  Ikiwa na ongezeko la watu la wastani wa asilimia 2.0 kwa mwaka.

UTAWALA

Wilaya  imegawanyika katika Tarafa 4, Kata 25, Vijiji vilivyosajiliwa 125 na Vitongoji 477. Mchanganua wa kiutawala na idadi ya watumishi imeoneshwa katika jedwali 1 na 2

Jedwali 1. Mgawanyo wa Kiutawala

MWAKA

TARAFA

KATA

VIJIJI

VITONGOJI

2005

4

15

101

452

2010

4

18

121

463

2015

4

25

125

477

Wilaya ya Mkuranga ina jumla ya Madiwani 35 kwa mchanganuo ufuatao:- Mbunge wa kuchaguliwa mmoja (1), Madiwani 25 wa kuchaguliwa na Madiwani 8 wa Viti Maalum. 

Jedwali 2. Hali ya Watumishi kwa kipindi cha miaka   sita (6)

MWAKA
MAHITAJI
WALIOPO
UPUNGUFU
2009
1513
1319
194
2010
2,057
1,644
413
2011
2,057
1,661
396
2012
2315
2014
301
2013
2353
2089
264
2014
2555
2302
253
2015
2929
2623
306
2016
3506
2719
787

SHUGHULI ZA KIUCHUMI ZA WAKAZI WA WILAYA YA MKURANGA.

Kilimo ni shughuli kuu ya kiuchumi kwa wananchi wa Wilaya ya Mkuranga.  Inakadiriwa kuwa kiasi cha 85% ya wakazi wa Wilaya ya Mkuranga wanajishughulisha na Kilimo hususan kilimo cha Korosho, Nazi na aina mbalimbali za matunda kama mazao ya biashara.  Kiasi cha wakazi waliobaki 15% hujishughulisha na shughuli nyingine zikiwemo, Uvuvi, Uvunaji wa mazao ya misitu, Biashara ndogo ndogo na ajira za ofisini.

Tofauti na mazao ya biashara, wakazi wa Wilaya ya Mkuranga hujishughulisha na kilimo cha mazao ya chakula kama vile Muhogo, Mpunga, Mahindi, Viazi vitamu na mazao ya jamii ya kunde. 

2.1       HUDUMA ZA JAMII

Huduma za jamii zilizomo Wilayani ni pamoja na elimu iliyotolewa katika Shule za Msingi 116,(kati ya hizo Shule 111 ni za Serikali na 5 ni za binafsi). Shule za Sekondari 33, kati ya hizo 22 ni za Serikali na 11 ni za binafsi.Vituo 42 vya kutolea huduma ya Afya, na huduma ya usambazaji wa maji safi na salama inayotolewa katika vikao asilimia 54 ya wakazi wote wanaokadiriwa kufikia 223,573.Aidha, Kufikia mwezi Julai, 2015, huduma hizi za jamii bado zinatolewa kwa kiwango cha chini ya mahitaji kutokana na uwezo mdogo kifedha na miundo mbinu hafifu/duni iliyopo Wilayani hivi sasa.

Matangazo

  • TANGAZO LA MKUTANO WA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI February 14, 2018
  • Tangazo la Matokeo ya Kidato cha IV February 03, 2018
  • Tangazo la Zabuni February 06, 2018
  • TAMASHA LA MICHEZO December 22, 2017
  • Tazama vyote

Habari Mpya

  • Migogoro itatuliwe na Watendaji ngazi za kata-DED Munde

    April 18, 2018
  • wananchi Mkuranga wapanda miti 500,000

    April 13, 2018
  • Wazazi,walezi wasiowapeleka watoto Shule kuchukuliwa hatua

    March 10, 2018
  • Mbunge Hawa Mchafu awaasa wana Jamii kujiepusha na vitendo viovu

    March 09, 2018
  • Tazama vyote

Video

Ajali ya Basi na Hiace Mkuranga
Video Zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Fomu ya Ruhusa ya Ugonjwa kwa Watumishi (Sick Sheet Form)
  • FFARS user manual
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Barua pepe za ofisi za watumishi
  • Fomu ya Likizo kwa Watumishi
  • Fomu ya Ruhusa kwa Watumishi
  • Fomu ya Maombi ya Leseni ya Biashara
  • Fomu za Maombi ya Kiwanja

Tovuti Linganifu

  • TAMISEMI
  • e-GA
  • OR - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Ajira
  • Ikulu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Baraza la Mitihani la Tanzania
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga

    Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania

    Telephone: +255232110038

    Simu ya Mkononi: +255784494689

    Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma zetu

Hatimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga.Haki zote zimehifadhiwa