Afya na Ustawi wa Jamii
UTANGULIZI
Idara ya Afya inatekeleza majukumu yake kwa kufuata miongozo inayotolewa na Wizara ya afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga ina hospitali moja ya wilaya (Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga. Pia ina vituo vya afya sita(6) ambavyo ni Mkamba, Kisiju,Nyota ya bahari,St Irene Kilimahewa, St Vicent-Vikindu na Ibun Jazar-pia kuna zahanati 54.
Idara imelenga kutoa matibabu kwa gharama nafuu kwa wananchi wa Mkuranga.
MAJUKUMU YA IDARA
Kutoa huduma za matibabu na uuguzi kupitia vituo vya afya, zahanati na hospitali ya wilaya. Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga inatoa huduma za upasuaji mkubwa na mdogo ambazo hutolewa kwa wagonjwa wa nje na wa kulazwa.
Kukagua dawa na vifaa tiba kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.
Kusimamia manunuzi ya dawa, vitenganishi vya maaabara,vifaa na vifaa tiba kwa ajili ya kuvisambaza vituo vya huduma za afya.
Kupitia Ustawi wa jamii idara inatoa huduma za kuzuia ukatili wa kijinsia na ukatili kwa watoto.
Kukagua maabara na kuhakikisha zimesajiliwa na zinatoa huduma bora kwa mujibu wa miongozo ya Wizara.
Kusajili maduka ya dawa na vipodozi, kuyakagua mara kwa mara ili kuhakikisha yanafuata sheria, kanuni na miongozo.
Kuratibu huduma za afya ya uzazi na mtoto zikiwemo na uzazi salama, huduma za chanjo kwa watoto chini ya miaka mitano, wajawazito na uzazi wa mpango.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.