MISITU:
Halmashauri ya ina Jumla ya misitu ya Hifadhi 19 yenye ukubwa wa hekta 12,256.54, kati ya hiyo,misitu minne (4) ni ya serikali kuu,ambayo ni;
1.Masanganya
2.Mkerezange
3.Vikindu- utalii ikolojia unafanyika
4.Misitu ya mikoko
Misitu 15 ni misitu ya Hifadhi ya vijiji ambayo ipo katika mpango wa usimamizi shirikishi(PFM) Misitu hii ipo katika vijiji vya Vianzi,Chamgoi,Mkuruwili,Mpafu,Mkanoge,Kibudi,Kibesa,Mkiu,Mvuleni,Kilamba,Kibuyuni,Kerekese,Misasa,Mbezi Mlungwana na Kifumangao.
Misitu hii inaweza kutumika kwa shughuli Rafiki na mazingira kama utalii ikologia,kama unavyofanyika katika msitu wa Vikindu,ufugaji wa nyuki,mafunzo,tafiti,matambiko nk.
Upo uvamizi unaopelekea kuharibika na hata kupotea kwa misitu hii.Shughuli za kibinadamu zinazoathiri misitu hii ni pamoja na ukataji wa miti kwa ajili ya kufungua mashamba,ukataji wa kuni na majengo,uchomaji wa mkaa,uingizaji wa mifugo kwa ajili ya malisho,uchomaji moto ovyo na kufanya makazi ndani ya misitu.
Zipo jitihada mbalimbali zinazofanyika kupambana na uharibifu wa misitu katika wilaya yetu ikiwa ni pamoja na;
1.Kufufua mipaka ya misitu hii ambayo kwa sasa aionekani vizuri
2.Kutoa elimu ya uhifadhi wa misitu na utunzaji wa mazingira kwa jamii inayozunguka mae
neo ya misitu hii.
3. Kufanya doria za kudhibiti uharibifu wa makusudi wa misitu.
4. Kupanda miti ili kurudishia miti iliyokatwa katika misitu hii
5.Kuzima moto mara tu unapojitokeza katika misitu hii.
UZALISHAJI WA MICHE YA MITI
Zipo bustani za miche ya miti mbili (2) ambazo zinamilikiwa na Halmashuri ya Wilaya moja na nyingine ina milikiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS).
Bustani hizi zinazalisha miche ya miti ya aina mbalimbali pamoja na miche ya matunda,kivuli na mapambo.Ambapo miche inayozalishwa hutolewa kwa Taasisi za Serikali na za binafsi kama,shule,vyuo.makanisa,misikiti,Ofisi nk,na pia kwa watu binafsi wenye uhitaji.Miche hii pia hupandwa katika misitu yetu ya Hifadhi.Miche inayozalishwa hutolewa bure bila ya malipo.
Na |
Aina ya makazi ya Wanyama
|
Aina ya Wanyama waliopo
|
Kijiji
|
Kata
|
Tarafa
|
1 |
Bwawa la Kikulwi
|
Kiboko na Mamba
|
Kisayani
|
Mbezi
|
Shungubweni
|
2 |
Mto Kogamimba
|
Mbamba na Kiboko
|
Mfurumwambao
|
Vianzi
|
Mkuranga
|
3 |
Mto Mbezi
|
Mamba
|
Mbezi
|
Mbezi
|
Shungubweni
|
4 |
Bwawa la Manze
|
Kiboko
|
Mwarusembe
|
Mwarusembe
|
Mkamba
|
5 |
Bwawa la Ziziwa
|
Kiboko
|
Mpafu
|
Dondo
|
Kisiju
|
6 |
Bwawa la Ruvungwi
|
Kiboko
|
Kilimahewa
|
Nyamato
|
Mkamba
|
8 |
Bwawa la Zakwati
|
Kiboko
|
Misasa
|
Lukanga
|
Kisiju
|
9 |
Mto Msambanyamani
|
Mamba
|
Mavunja
|
Kisiju
|
Kisiju
|
WANYAMAPORI:
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.