Kitengo cha ufugaji nyuki kina mpango wa kuhakikisha wananchi wa Mkuranga wanafanya ufugaji nyuki na fursa zake kama chanzo kikuu cha uchumi mpaka 2030. Katika kutekeleza mpango huo wa miaka kumi kitengo kilianzaisha kampeni inayoitwa NYUKI NI FURSA TUITUMIE iliyozinduliwa tangu mwaka 2019 kwa nia ya kutoa elimu na kuhamasisha fursa za nyuki Mkuranga. Kampeni hii inakauli mbiu tofauti totuti kila mwaka kulingana na hatua na mahitaji. Mwaka huu 2021 Nyuki ni fursa inakauli mbiu ya tunapiga hatua na tunaendelea kupiga hatua.
Kitengo cha ufugaji Nyuki kupitia kampeni hii ya Nyuki ni FursaTuitumiekimefanikiwakupigahatuakatika mambo yafuatayo
Kutoka kuvunatani 1 mwaka 2019mpakatani 8 mwaka 2021.
Pamoja na hayo tumefanikiwa kuongezea ujuzi wa kutengeneza mizinga kitaalam kwa vitendo kwa mafundiseremala 5 hivyo kuwa na uhakika wa viwandavidogo vya kutengeneza mizinga ya kisasandani ya wilaya yetu.
Kampeni ya Nyuki ni fursa kupitia wawezeshaji mbalimbali kama SONGAS imewezesha fursa ya kilimo nyuki imeanzakutekelezwa kwa wadau wa ufugaji nyuki.
Mafanikio mengine ni kuweza kupata fursa ya mafunzo ya kuongeza thamani mazao ya nyuki na mnyororo wa thamani kwa kushirikiana na SIDO kwa vikundi 7 vya ufugaji nyuki na ujasiliamali.
Kitengo kinatoa wito kwa wananchi wa Mkuranga kufanya shughuli za ufugaji nyuki ikiwa ni pamoja na utunzaji wa mazingira kuondokana na majanga ya kimazingira. Pia kitengo kinapendekezakujikita katika fursa ya kilimo nyuki kwa ajili ya kupata mazao yenye ubora na faida mara mbili.
Kitengo kinakaribisha wadau wote kwa ajili ya kujipatia elimu ya ufugaji nyuki na fursa zake ikiambatana na uwezeshaji panapowezekana.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.