Kumuhamisha Mwanafunzi wa shule ya Msingi
Ili kumuhamisha mwanafunzi wa shule ya Msingi kutoka shule moja kwenda nyingine hatua zifuatazo zinapaswa kufuatwa na mzazi/mlezi:-
1. Mzazi/Mlezi atatakiwa kufika shule anayosoma mwanafunzi na kujaza fomu za uhamisho pamoja na kuchukua kadi ya maendeleo ya mwanafunzi ambayo pia sharti ijazwe na isainiwe.
2. Mzazi/Mlezi atawasilisha shuleni picha sita za pasipoti.
3. Fomu na kadi ya maendeleo ya Mwanafunzi zitasainiwa na mwalimu wa darasa, mwalimu Mkuu Msaidizi na mwalimu Mkuu. Baada ya fomu za uhamisho na kadi ya maendeleo ya mwanafunzi kusainiwa katika ngazi ya shule zitapelekwa kwa mratibu elimu Kata kusainiwa.
4. Baada ya fomu za uhamisho kusainiwa katika ngazi ya Kata itapelekwa na mzazi/mlezi katika ofisi ya afisa elimu wa Halmashauri kwa ajili ya kupitishwa na kusainiwa.
5. Fomu za uhamisho zilizosainiwa na afisa elimu zitapelekwa katika ngazi ya mkoa kupitishwa na kusainiwa an afisa elimu Mkoa. Baada ya kupitishwa na kusainiwa na afisa elimu mkoa fomu hizo zitapelekwa mkoa mwanafunzi anapohamia na kufuata utaratibu tajwa hapo juu isipokuwa kwa upande wa Mkoa mwanafunzi anapohamia taratibu zitaanzia ofisi ya afisa elimu aMkoa kushuka chini.
Angalizo:Ikiwa mwanafunzi anahama kutoka shule moja kwenda nyingine ndani ya Wilaya, taratibu za uhamisho zitaishia ofisi ya afisa elimu wa Wilaya.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.