UTARATIBU WA KUPATA LESENI MPYA
1.Chukua barua ya utambulisho kutoka kwa Afisa Mtendaji wa kijiji
2.Jaza fomu ya maombi kutoka kwenye tovuti ya Halmashauri ambayo ni www.mkurangadc.go.tz au fomu uliyopewa katika ofisi za Biashara Wilaya.
3.Fomu iliyokamilika irudishwe ikiwa na nakala zifuatazo
a.-Cheti cha TIN ya TRA na Tax clearance kutoka TRA
b.-Nakala ya vibali vya mamlaka husika na biashara unayotaka kufanya kama vile TFDA(Maduka ya dawa na chakula) EWURA(vituo vya mafuta nk)
4.Baada ya kukamilisha hayo,utasajiliwa kwenye mfumo wa mapato wa Halmashauri na kupewa bili
5.Utalipia malipo ya bili hiyo benki ya NMB tawi la Mkuranga (Usilipie kwa wakala wala tawi lingine)
a.Halafu utarudi Halmashauri na Ankara ya benki
6.baada ya hapo utapata leseni yako halali ya biashara na risiti halali
7.UTARATIBU WA KUHUISHA(RENEWAL) LESENI ILIYOISHA MUDA WAKE(EXPIRE)
1.jaza fomu ya maombi ya kuhuisha leseni
2.fomu iliyojazwa kikamilifu irudishwe ikiwa na leseni iliyoisha muda wake na tax clearance na TRA
3.utapewa bili na kwenda nayo Benki ya NMB tawi la Mkuranga kulipia(usilipe kwa wakala wala tawi lingine)
4.baada ya malipo utarudi Halmashauri na Bank slip na kupewa risiti na leseni halali.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.