Kilimo na Umwagiliaji
Kusimamia utoaji wa huduma bora za ugani kwa wananchi, Kuhimiza wakulima kujiunga katika vikundi ili kuwa na nguvu ya pamoja, Kuhamasisha wakulima kufuata mbinu bora zinazopendekezwa kitaalamu katika shughuli za uzalishaji, Kuwafikishia wakulima teknolojia mpya baada ya kufanyiwa utafiti na kuthibitishwa, Kuwezesha wakulima kutambua fursa na vikwazo vilivyopo kwa maendeleo ili kuwapelekea teknolojia kulingana na mahitaji yao, Kupendekeza, kuandaa na kusimamia utekelezaji wa sheria ndogo ndogo za kilimo (Agricultural By-laws) kwa kushirikiana na watendaji wengine ndani ya wilaya, Kuhamasisha sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika kutoa huduma za ugani ndani ya wilaya, Kuratibu na kusimamia maandalizi ya makisio ya mahitaji ya pembejeo na zana za kilimo, upatikanaji na usambazaji wake, Kutoa taarifa ya milipuko ya magonjwa na wadudu waharibifu kwa kuwasiliana na uongozi wa wilaya, mkoa, kanda na wizara za sekta ya kilimo.
Kuwashauri wakulima namna ya kupambana na wadudu, magonjwa na magugu ya mimea mashambani mwao, Kutafuta taarifa za masoko na kuzifikisha kwa wakulima, Kuhamasisha na kuimarisha mitandao ya wakulima, Kutambua (kwa kuorodhesha) watoa huduma za ugani wa sekta binafsi, Kuandaa na kuitisha mikutano ya wadau wa sekta ya kilimo angalau mara moja kwa mwaka, Kufuatilia teknolojia za kuendeleza mazao muhimu katika wilaya hii kutoka katika vituo vya utafiti na kuwawezesha wataalamu katika wilaya kuzielewa ili zitumike kwa usahihi, Kushirikiana na watafiti katika kujaribu teknolojia mpya katika mashamba ya wakulima ndani ya wilaya
Ushirika
Kuhamasisha uanzishwaji na uendelezaji wa Vyama vya Ushirika wa aina mbalimbali kulingana na mahitaji ya jamii, Kuhimiza uimarishaji wa mitaji katika vyama vya Ushirika na kuhakikisha vyama vinafanya shughuli zake za biashara kwa kujitegemea
Kutambua na kusaidia juhudi za vikundi vya wazalishaji wadogo kwa lengo la kuviwezesha kuwa vyama vya ushirika imara kiuchumi baadaye, Kuhakikisha kuwepo kwa uongozi na menejimenti yenye uwezo wa kusimamia ushirika kibiashara na ambayo inawajibika kwa wanachama, Kuelimisha jamii kuhusu ushirika ulivyo na manufaa yake kwa wanachama kwa kutumia Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika
utoa mafunzo ya uendeshaji na utawala kwa Vyama vya Ushirika, Kufanya ukaguzi wa Hesabu za Vyama vya Ushirika na kusoma taarifa kwa wanachama, Kukusanya Takwimu za Vyama vya Ushirika na kuziwasilisha Mkoani kila robo mwaka, Kusaidia kukusanya Mapato ya Halmashauri kupitia Vyama vya Ushirika, Kumshauri Mkurugenzi Mtendaji juu ya uendeshaji wa Vyama vya Ushirika.
Kupata kazi mbalimbali zinazofanywa na Idara ya Kilimo bonyeza hapa TAARIFA ZA TOVUTI -KILIMO.pdf
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.