Kutafsiri na kusimamia sheria, kanuni, sera, miongozo na taratibu mbalimbali za sekta za mifugo na uvuvi kitaifa ili kuhakikisha uwepo wa uzalishaji endelevu wa mifugo na mazao yatokanayo na mifugo na uvuvi katika wilaya kwa madhumuni ya kufikia malengo ya uzaalishaji kitaifa; Kushirikiana na wadau/washirika wa maendeleo (kama vile Taasisi binafsi na za umma) katika kutoa huduma shirikishi za ugani, kuanzisha na kuendeleza miradi ya uendelezaji mifugo na uvuvi katika wilaya; Kushirikiana na uongozi katika ngazi mbalimbali za kitaifa, Mkoa, Halmashauri na Idara nyingine katika kutimiza majukumu ya kila siku; Kushirikiana na wadau mbalimbali kudhibiti uingiza wa mifugo kiholela na kuzuia uvuvi haramu katika wilaya, kwa kufanya doria, kutoa leseni za uvuvi na kutoa elimu juu ya matumizi bora ya zana za uvuvi.
Kushauri na kuzisimamia serikali za vijiji kutenga maeneo ya malisho ili kuzuia migogoro inayoweza kutokea baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi katika vijiji; Kuwa daraja kati ya wafugaji na watafiti wa mifugo na uvuvi, kwa kuzitambua na kuchukua changamoto za wafugaji na kuzipeleka kwa watafiti ambao watazitafutia majibu muafaka na kurudisha/ kupeleka mrejesho kwa walengwa. Pia kusambaza teknolojia sahihi za kitaalam kutoka kwa watafiti kwenda kwa wafugaji ili kuongeza tija katika uzalishaji wa mifugo, samaki na bidhaa zake; Kudhibiti magonjwa mbalimbali ya mifugo, ikiwemo yale ya mlipuko na yale yanayo waathili binadamu kutoka kwenye mifugo, kama vile Kifua Kikuu, Kimeta, Kichaa cha Mbwa n.k, kwa kutoa tiba, chanjo, ukaguzi wa nyama na kutoa vibali vya kusafirisha mifugo. Pia kutoa taarifa za magonjwa ya milipuko, kuchukua na kupeleka sampuli za wanyama katika kituo cha uchunguzi wa mifugo Temeke Dar es salaam; Kuhakikisha wataalam wa mifugo na uvuvi wenye sifa zinazo stahili wapo wa kutosha katika ngazi zote na wanahamasa ya kufanya kazi;
Kudhibiti ubora wa bidhaa za mifugo na uvuvi, pia kuhamasisha uongezaji thamani wa mazao ya mifugo na uvuvi na kusisitiza ufugaji wa kibiashara; Kutafsiri na kuunganisha majukumu, matakwa na malengo ya wadau watoa huduma za ugani katika sekta za mifugo na uvuvi; Kutambua aina ya wafugaji na mahitaji yao muhimu katika maeneo mbalimbali; Kuendeleza matumizi ya mbinu za asili za ufugaji; Kuendeleza na kuboresha kosaafu za mifugo ya asili kwa uhamilishaji na kutumia madume bora ili kuongeza uzalishaji wa mifugo; Kukuza na kuimarisha mitandao miongoni mwa wadau wa kutoa huma za ugani na wafugaji wenyewe; Kukuza ushiriki wa wadau binafsi wa kutoa huduma za ugani, kutunza kumbukumbu na kufuatilia shughuli zao; Kwa kushikiana na wadau wa maendeleo Kuwezesha ujenzi wa miundombinu ya mifugo na uvuvi katika maeneo ya wafugaji; Kukusanya, kuchambua, kutunza, kuboresha na kuzitumia taarifa/takwimu za mifugo na uvuvi katika kupanga mipango ya maendeleo na bajeti ya sekta katika wilaya; Kuhusisha na kushughulikia maswala mtambuka kama vile jinsia, mazingira na VVU/UKIMWI.
MAFANIKIO YA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI
Kutenga maeneo ya malisho
CHANGAMOTO
Wananchi kushindwa kumudu gharama za madawa, chanjo, viuadudu kutokana na vitu hivyo kuuzwa kwa bei kubwa na hakuna ruzuku inayotolewa na serikali, vilevile dawa au chanjo zinapatikana maeneo ya mbali hivyo kuongeza gharama za usafiri.
Upungufu wa miundombinu ya mifugo kama vile Majosho ya mifugo, Malambo na Vituo vya Huduma za Afya za Mifugo.
Uwepo wa mimea yenye Sumu
Ufinyu wa bajeti
Wafugaji wavamizi kutoka nnje ya Wilaya ya Mkuranga.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.