Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji ni idara inayohusika na masuala ya Kuratibu Mipango yote, Utekelezaji, Usimamizi na tathmini ya miradi ya Maendeleo katika halmashauri pamoja na kuandaa za bajeti ya Halmashauri.
Idara ya Mipango pia inashughulika na Kuandaa taarifa za utekelezaji kwa kila robo ya mwaka ikihusisha taarifa ya miradi,fedha na hatua za utekelezaji. Kuandaa taarifa ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama kwa Kila miezi sita, Kuandaa taarifa za Mafanikio za Serikali iliyoko madarakani, Kuandaa Mpango kazi wa utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo (Action Plan) na Kutoa taarifa za fursa za uwekezaji ndani ya Halmashauri.
USIMAMIZI WA MIRADI.
Idara ya mipango kwa kushirikiana na idara zenye miradi inawajibika kusimamia miradi kuanzia ngazi ya halamashauri hadi ngazi ya vijiji kwa kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara wa miradi hiyo. Utekelezaji wa miradi katika halmashauri inatokana na vyanzo mbalimbali vya fedha ikiwemo ruzuku serikali kuu, mapato ya ndani na wahisani.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.