Katika kuiendea siku ya maadhimisho ya sherehe za Miaka 61 ya uhuru, Watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga pamoja na vyombo vya usalama leo wameshiriki kufanya usafi katika Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga.
Zoezi hilo la usafi likiongozwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkuranga Bi. Veronika Kinyemi na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bi. Arafa Halifa walishiriki pia katika zoezi la upandaji wa Miti zaidi ya 100 katika eneo hilo la Hospitali.
Akiongea na watumishi hao Katibu Tawala huyo amemtaka Mganga Mkuu wa wilaya ya Mkuranga Bw. Ally Mbikilwa Kuhakikisha Miti hiyo iliyopandwa inasimamiwa na kutunzwa vizuri ili kufanikisha lengo lililokusudiwa la utunzaji wa Mazingira.
Aidha amemtaka Kaimu Mkurugenzi kuendelea kusimamia zoezi la watumishi kuishi katika Vituo vyao vya kazi ili kufanikisha utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa Majaliwa sambamba na kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananachi kwa urahisi.
Wilaya ya Mkuranga inatarajia kufanya sherehe za Miaka 61 ya uhuru katika Kijiji cha Miteza Kata ya Njia Nne siku ya Trehe 09/12/2022.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.