Kamati ya Siasa Mkoa wa Pwani leo imefanya ziara Wilayani Mkuranga ya kutembelea miradi mbalimbali ikiwemo barabara ya Mkuranga-Kisiju na kiwanda cha Lodhia group of Companies.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani Mh Ramadhani Maneno alisema “Serikali ya CCM ni sikivu wakati tunaomba ridhaa tulieleza nini tutafanya tukiingia madarakani ikiwemo miundombinu ya barabara Mkuranga-kisiju na maandalizi ya Mkuranga kupata Mji mdogo”.
Ramadhani aliongeza kwamba Maandalizi ya kupata Mji mdogo yapo kwenye ilani ya Chama Cha Mapinduzi ila kuna marekebisho yanahitajika na baada ya kurekebishwa ukifika wakati wa kufanya maamuzi ya kwenye Miji midogo Mkuranga nayo ipate hadhi ya kuwa na Mji mdogo.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng Evarist Ndikilo alisema katika wilaya ya Mkuranga watakagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi,walianzia Mafia, Rufiji kibiti kwa lengo la kukagua miradi inayotekelezwa na Serikali.
“Barabara ya Mkuranga mpaka kisiju ipo kwenye ilani ya uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi na mimi kama Mkoa ndio mtekelezaji wa ilani hii. 2015-2020 na nimeaminiwa na Mh Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli nitekeleze ilani”
Ndikilo alisisitiza kwamba wamekuja kukagua yale ambayo Chama iliahidi ikiwemo ujenzi wa barabara ya Tanroad ambapo kwa bajeti ya 2018/2019 imetengwa bil 23 kwa Mkoa mzima ikiwemo barabara ya Mkuranga.
Ndikilo aliongeza kwamba Barabara imejengwa kilomita 1.8 na imeongezewa kilomita tano na baadae Serikali itaongeza kilomita 45 ili ifike hadi Kisiju.
Aidha Ndikilo alisema “barabara hii ni muhimu sana sababu inaenda kata ya Mbezi ambapo kuna geti valve ya gesi namba 13 mlango wa kutolea gesi na gesi ni muhimu sana katika uwekezaji na uendelezaji wa viwanda”.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mh Filberto Sanga alisema barabara ya Mkuranga-Kisiju kilomita 1.8 imetumia tshs bil 1.8 lakini Serikali inakusudia kuendelea na ujenzi mwingine wa kilomita tano ambazo zitaongezeka.
Kamati ya Siasa Mkoa wa Pwani imefanya ziara ya siku moja Wilayani Mkuranga ya kutembelea miradi mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo barabara ya Mkuranga-Kisiju kilomita 1.8 na kiwanda cha Lodhia group of Companies
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.