Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga limeketi kwenye Mkutano wa kujadili taarifa za Robo ya Pili kwa Mwaka wa Fedha 2023-2024.
Akizungumza kwenye Mkutano huo ambao umefanyika leo Februari 14, 2024 katika ukumbi wa Flex Garden Kiguza , Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Waziri K. Kombo amepongeza hatua za maendeleo ndani ya Halmashauri na kusema kuwa ukusanyaji wa mapato kwa robo hizi mbili ni Tsh. Bilioni 6.5 sawa na asilimia hamsini (50%) za kiwango cha ukusanyaji ambapo asilimia 60% ya fedha hizo inaenda kwenye miradi ya maendeleo.
Aidha Mkutano wa Baraza hilo la Madiwani umeridhia maombi ya kuipandisha hadhi Halamshauri ya Wilaya ya Mkuranga na kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Mkuranga wakati utaratibu mwingine ukisubiriwa kufuatwa.
Akizungumza juu ya ombi hilo Diwani wa Kata ya Tengelea Mhe. Shabani H. Manda amesema endapo Wilaya ya Mkuranga ikifanikiwa kupanda hadhi na kuwa Manispaa itasaidia kutatua changamoto mbalimbali za Wananchi kwa sababu idadi ya watu inazidi kuwa kubwa na mahitaji ya huduma yanazidi kuongezeka.
Akiongezea kwenye hilo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mohamed S. Mwera amesema endapo Ombi hilo likikubaliwa basi wananchi wategemee miradi mikubwa ya maendeleo ndani ya Halmashauri hii ya Wilaya ya Mkuranga.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.