Mkutano maalum wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga limetoa pongezi kwa Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kupeleka Fedha nyingi za Maendeleo katika Sekta za Elimu na Afya ndani ya Wilaya hiyo.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo Mohamed Mwela Alipokuwa anafunga Mkutano uliofanyika jana kwenye ukumbi wa Flex Garden Kiguza Mkuranga.
“Mkuu wa Wilaya tunaomba utufikishie salamu zetu kwa Mh. Rais Samia Suluhu Hassan kuwa tunaendelea kumpongeza na kumshukuru kwa kuwapenda watoto wa Mkuranga” alisema Mwenyekiti huyo.
Akiwasilisha taarifa ya Uendelezaji wa ujenzi wa Madarasa Mapya ya sekondari 132 baada ya kupokea Fedha za awali Shilingi Bilioni 2.64, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bi. Mwantum Mgonja amesema Halmashuri ya Mkuranga imepokea Fedha nyingine kutoka Serikali kuu Shilingi Bilioni 1.8 kwa ajili kuendeleza na kuimarisha miradi ya Elimu na Afya ndani ya Wilaya hiyo.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Bi. Khadija Nasr Ali, akijibu hoja ya Vikao kazi hapo awali, amesema amelipokea lakini ataendelea kufanya kazi kwa mujibu wa Sheria na taratibu zilizopo na kwa njia ambazo ataona inafaa na amesisitiza kuwa Milango ya Ofisi yake iko wazi na yuko tayari kupokea ushauri wowote utakaoleta tija kwa manufaa ya wanachi wa Mkuranga.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.