Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga lifanya Mkutano wake wa kujadili na kupitisha taarifa za Kata Robo ya nne kwa Mwaka wa fedha 2023-2024.
Mkutano huo uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Flex Garden Kiguza umepitia taarifa za Kata zote 25 zilizopo katika Wilaya ya Mkuranga.
Miongoni mwa taarifa zilipitishwa kupitia taarifa hizo ni pamoja utekelezaji wa Miradi, ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri na chamgamoto zinazojitokeza katika kutekeleza shughuli za maendeleo.
Mkutano huo umeongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Mohamedi Maundu pamoja na Katibu wake Patrick Saduka ambaye ni Afisa rasilimali watu kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mkuranga
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255222928730
Simu ya Mkononi: 0634329394
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2026 MkurangaDc. All rights reserved.