Tumieni mikopo ya asilimia kumi kujiletea maendeleo - DED Mkuranga
Mkurugenzi mtendaji Hamashauri ya wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani Bi. Mwantum Mgonja amewaasa wanawake wanaonufaika na Mikopo ya asilimia 10 inayotokana na mapato ya ndani kuitumia kwa weledi kwa lengo la kuinua vipato vyao na kuboresha hali ya maisha.
Bi. Mgonja amewaasa wanawake hao leo wakati alipotembelea banda la Halmashauri hiyo kwenye maonesho ya nane nane Kanda ya Mashariki yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere Mjini Morogoro kwa lengo la kujifunza na kujionea shughuli mbali mbali zinazoendelea katika banda hilo.
"Natoa rai kwa wanufaika wa mikopo hii ya asilimia 10 waweze kuitumia fursa hii na kuanzisha biashara endelevu hatimae kujikwamua kiuchumi,” amesema Bi. Mgonja.
Aidha Mkurugenzi huyo ametumia fursa hiyo kuwakaribisha watanzania wote wanaoingia katika viwanja vya maonesho kufika katika banda la mkuranga na kujifunza shughuli zinazoendelea.
Maonesho ya 88 kanda ya Mashariki yamepambwa ka kauli mbiu isemayo Ajenda ya 10/30 kilimo ni biashara shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo, Mifugo na uvuvi.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.