Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Bi.Mwantu Mgonja ameeongozana na Wataalam wa Halmashauri ya Wilaya Mkuranga(Afisa Mipango,Mweka Hazina,Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi,Mtendaji wa Kata ,Maafisa Ugani,pamoja na Mtendaji wa Kijiji ) wamefika katika Shule ya Msingi Kisiwani (Shikizi) iliyopo katika Kijiji cha Mipeko Kata ya Mipeko.
Katika kikao kazi hicho wamekutana Viongozi wa Kijiji,Wajumbe wa Kamati ya Shule pamoja na Wananchi kwa lengo la kujadili na kutatua changamoto zilizopo katika Shule hiyo.
Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga kupitia Mapato ya Ndani 2022/2023 tayari imetenga Fedha kwaajili ya kujenga vyumba viwili vya Madarasa na Matundu 10 ya Vyoo
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255222928730
Simu ya Mkononi: 0634329394
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2026 MkurangaDc. All rights reserved.