Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Bi.Mwantum Mgonja ameongozana na Mhe.Ally Mbwera Diwani wa Kata ya Njia Nne,Mtendaji Kata,Wataalam mbalimbali wa Kata pamoja na Watendaji wa kijiji na kufika katika kijiji cha Miteza na Kijiji cha Njia Nne kwaajili ya kutembelea miradi ya maendeleo na kuhamasisha Maendeleo ya Kata pamoja na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Kata ya Njia Nne.
Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mwaka wa Fedha 2022/2023 kupitia Mapato yetu ya Ndani tumetenga Shillingi Millioni 30 kwaajili ya umalizaji wa Zahanati ya kijiji cha Miteza.
Aidha amewahamasisha wananchi wote Tarehe 23 Agost kujitokeza kuhesabiwa na kutoa ushirikiano kwa Makarani watakaofika kwaajili ya kuchukua taarifa
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255222928730
Simu ya Mkononi: 0634329394
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2026 MkurangaDc. All rights reserved.