Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri wa Wilaya ya Mkuranga Bi.Mwantum Mgonja amefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ameongozana na Wakuu wa Idara ya Elimu Sekondari,Afisa Maendeleo ya Jamii,Afisa Mipango,Afisa manunuzi,Mganga Mkuu wa Wilaya,Afisa Mhifadhi Mazingira na Taka,Mhandisi wa Wilaya,Mwandishi wa Mikutano pamoja na Afisa Habari na kufika katika kijiji cha Kisegese na kukagua mradi wa kituo cha Afya na Shule ya Sekondari ya Kisegese.
Bi.Mwantum Mgonja amezuia kutumika kwa matofali 10,126 ambayo yapo chini ya kiwango yaliyokuwa katika ujenzi wa kituo cha Afya cha Nyamato Kata ya Nyamato Kijiji cha Mvuleni ujenzi wake ambao unagharimu kiasi cha shilingi Mill.400 ambayo ni mapato ya ndani ya Halmashauri.
Aidha amewataka wazabuni wa Local fundi wote waliopata kazi za ujenzi wa miradi ambayo ipo ndani ya Halmashauri kuwa makini na fedha za Serikali na kisisitiza kuwa wale wote wanaoharibu miradi kutokupata kazi tena ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.