Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Bi.Mwantum Mgonja pamoja na Wataalam wa Elimu Msingi wamefanya kikao kazi na Kamati ya Shule ya Msingi Ngunguti iliyopo kata ya Mkuranga pamoja na Walimu wa shule hiyo lengo likiwa kutatua changamoto na kuhakikisha wanaleta malezi bora kwa wanafunzi hao.
Katika kikao hiko Kamati ilipata fursa ya kuelezea changamoto zinazoikabili shule ikiwemo ya upungufu wa Walimu kwani walimu waliokuwepo ni wachache ukilinganisha na idadi ya wanafunzi waliopo.
Changamoto nyingine waliyoibainisha ni shule kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi hivyo kupelekea miundo mbinu kutokidhi idadi ya wanafunzi na hivyo kupelekea kushindwa kutoa huduma stahiki kwa wanafunzi.
Aidha kamati imeomba kupewa eneo jingine lenye uwezo wa kujenga shule mpya kwa lengo la kupunguza msongamano wa wanafunzi katika shule hiyo na kuahidi endapo watapata eneo basi watashirikiana na serikali katika ujenzi wa shule hiyo.
Nae Mkurungenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Bi.Mwantum Mgonja amewapongeza wanakamati hao pamoja na walimu kwa ushirikiano wao wa kuleta malezi bora kwa wanafunzi.
Aidha amewata kuandika barua ya kuhusu kupewa eneo la kujenga shule mpya na kufika ofisini kwake ili kuweza kufata taratibu zote na wahusika watalifanyia kazi.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255222928730
Simu ya Mkononi: 0634329394
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2026 MkurangaDc. All rights reserved.