Rai yangu kwa Wananchi wote wanaoendelea na ujenzi wa majengo mbalimbali ni kufuata taratibu za kisheria za ujenzi ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga ambazo zinawataka wananchi kuhakikisha kuwa wanapata vibali vya ujenzi kutoka Halmashauri ili kuwa na majengo bora na kuwawezesha makusanyo ya mapato ya ndani yatakayotumika katika ujenzi wa miundombinu.
Hayo ameyasema Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Bi.Mwantum Mgonja leo Juni 23, 2022 wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa majengo yaliyojengwa bila kufata utaratibu ikiwemo ukosefu wa vibali vya ujenzi.
Aidha ziara hiyo ilihusisha Maafisa kutoka idara ya Ujenzi na Ardhi na Kata zilizotembelewa ni Mwarusembe,Mkuranga,Mipeko,Vikindu na Mwandege.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.