Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga kupitia Idara ya maendeleo ya jamii imekutana na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) katika ukumbi wa Al-Rahmah development complex ikiwa na lengo la kupitia na kujadili taarifa za robo ya nne Aprili/ Juni 2022 za utekelezaji kazi za mashirika na serikali.
Akizumgumza wakati wa mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji bi. Mwantumu Mgonja ambaye ni Mgeni rasmi amewataka watendaji wa mashirika hayo kuwa na utaratibu wa kuwasilisha taarifa za mipango , malengo na utekelezaji wa shughuli zao katika dawati linaloratibu utendaji wao.
Aidha Bi. Mwantum hakusita kutoa shukrani zake za dhati kwa watendaji wa mashirika hayo kwa ushirikiano wao mzuri katika kuihudumia jamii kupitia shughuli mbali mbali wanazozitekeleza kwa kushirikiana na Halmashauri kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii.
Mwanamsiu Dosi Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii (W) alisema" NGOs zote zifanye kazi kwa kuzingatia sheria, miongozo na taratibu za serikali na kufata maelekezo anayotoa mratibu mara kwa mara kupitia vikao aidha aliwataka kuhuisha mtandao wao (MKUNGONET) na kushughulikia mgogoro wa uongozi uliopo.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.