Wakala wa usajili wa biashara na leseni (BRELA) ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani kwa kuhamasisha wafanyabiashara kujiandaa kuelekea mfumo wa mtandao
Akizungumza na wafanyabiashara wa wilaya hiyo kwenye ukumbi wa Flex Garden, Mkurugenzi wa utawala na fedha Bakari Ally Mketo alifurahishwa na mwitikio wao hali itakayofanikisha malengo kutimia
Mkurugenzi huyo aliweka bayana faida kutumia mfumo ni pamoja na kuondoa urasimu ,rushwa isiyo ya lazima hivyo itafanikisha serikali kuongeza mapato kupitia usajili huo
Akizungumzia changamoto ya upatikanaji wa vitambulisho vya taifa, alisema tayari wamekubaliana na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ili kila wilaya watenge dirisha la wafanyabiashara pia watatumia namba ya kitambulisho cha Taifa
Mketo alisema wamejipanga kuwa rafiki kwa wafanyabiashara kwa kuwekea gharama ndogo ya usajili shilingi aki 3 hadi 5 tofauti na wanasheria wanaotoza milioni 4
Zoezi hilo lililoanza desemba mwaka jana kanda zote limeeta tija kwa (BRELA) baada ya kuvuna wasajili (730) kutoka (62) hu akifurahia kutoa elimu kuwa wachache ili wakasambaze kwa wengi
Naye afisa biashara Michael Mpupua alipongeza ujio wa (BRELA) huku akiwataka watendaji wa vijiji kuhamasisha wafanyabiashara wajisajili
Mfanya biashara wa kijiji cha Vikindu ambaye pia ni mstaafu serikalini Judicate Ndossi alipongeza mafunzo hayo na kusema yatarahisisha kusajili kampuni zao waweze kuboresha biashara zao kisheria
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.