Diwani kata ya Tengelea ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga Mhe. Shaaban Manda amefanikisha kuanza kwa ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa 6 toka Kiguza mpaka Nyangolo
Akizungumza na wananchi waliojitokeza kwa wingi jana wakati wa kikao cha wazazi kilichofanyika katika shule ya msingi Hoyoyo, Manda alisisistiza kuwa barabara hiyo inayosimamiwa na wahandisi wa Tanzania Rural and Urban Road Agency (TARURA) itakuwa na kiwango cha hali ya juu sana
“lakini niwaambieni sasa jambo jema zaidi watamwaga kifusi ‘kikali’ kwenye kilomita hizo, lakini pia kulikua tuna tatizo sana kipindi cha masika eneo la mvemle itawekwa karavati jipya” alisema Diwani huyo mwenye kiu kubwa ya maendeleo.
Mbali na suala hilo, Manda pia alijitolea jumla ya daftari 100 na baiskeli kwa ajili ya watoto wenye ulemavu shuleni hapo.
Pia aliongeza nguvu katika zoezi kuingiza umeme shuleni hapo ambapo alichangia jumla ya Tsh. 200,000/- huku akitoa ahadi ya kuchangia jumla karatasi (rimpapers) bunda 10 na fedha taslimu 100,000/- kwa wanafunzi watakaofanya mtihani wa darasa la 7 ikiwa ni utaratibu aliojiwekea kusaidia jitihada za elimu
Aidha alipongeza jitihada za walimu, viongozi kamati shule na wazazi ambao wamesaidia kuifanya shule hilo kushika nafasi ya 7 kiwilaya katika matokeo ya darasa la saba msimu uliopita.
Wakiongea mara baada ya kikao hichowananchi waliohudhuria walimpongeza diwani huyo huku wakimtakia afya njema ili aendelee kuleta maendeleo zaidi katani hapo
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.