Changamoto za kupanga na kuandaa mpango wa bajeti katika ngazi za Vijiji na Kata zinaenda kutoweka baada ya watendaji wa kata na vijiji kupata mafunzo ya uandaaji wa Mipango na Bajeti
Mafunzo hayo yametolewa na kuratibiwa na divisheni ya miapngo na uratibu yamefanyika agosti 8, 2025 katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Mwinyi.
Aidha mafunzo hayo ya uaandaaji wa Mipango ya Bajeti kwa Maafisa Bajeti wa Vijiji na Kata Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga yana lengo la kuoanga vyanzo vya mapato na matumizi ndani ya Halmashauri ili kuhakikisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Akiongea baada ya kufungua Mafunzo hayo Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Waziri Kombo amesema mafunzo haya yataenda kupunguza au kuondoa kabisa changamoto za vijiiji vingi kutumia hela kidogo na kupakiwa na kiasi kikubwa cha hela na kupelekea kutumika kwa akaunti ya amana kufanya matumizi yao.
Mchakato huu wa uandaaji wa Bajeti ya Halmashauri ya mapato ya ndani unaongozwa na miongozo ya Serikali kupitia Ofisi ya Rais - TAMISEMI na Wizara ya Fedha.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.