Timu ya Wataalamu (CMT) ikiongozwa na Katibu Tawala Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani Bi Veronica Kinyemi leo imetembelea mradi wa Shule ya Msingi Chatembo iliyopo kata ya mwandege Kijiji cha Chatembo uliotekelezwa na Halmashauri kwa kutumia fedha kutoka Serikali Kuu kupitia mpango maalumu wa EP4R (EDUCATION PROGRAM 4 RESULT) zilizopokelewa Mwezi Juni 26,2020 na ujenzi kuanza katika kipindi cha robo ya pili Septemba-Novemba,2020
Akizungumza katika Ziara hiyo Katibu Tawala Bi, Kinyemi alipongeza timu ya wataalamu,wasimamizi wa mradi Pamoja na uongozi wa Shule ya Msingi Mwandege kwa kusimamia mradi kwa weledi na maarifa alisema, “mmeonesha kiwango kikubwa cha uaminifu mlichonacho na Imani ya kile mlichoaminiwa kukifanya hivyo nawapongeza sana na ninawataka sote kwa Pamoja tupambane kumalizia hapa palipobaki bila kuangalia tulipotoka ili Watoto wetu waweze kupata mahali pazuri pa kujipatia elimu ya msingi bila msongamano kama uliokuwepo awali”
Naye Mkuu wa shule ya msingi mwandege ambaye ni msiamizi wa mradi wa ujenzi, Ndg Azizi Mtwanga ambaye pia ni msimamizi waujenzi wa shule hiyo ya Chatembo alibainisha mafanikio ni Pamoja na kupunguza msongamano mkubwa wa wanafunzi waliokua wanaenda kusoma katika shule ya msingi mwandege na hivyo shule hiyo ikikamilika mwakani wanafunzi wengi watasajiliwa kwenye shule ya Msingi Chatembo .
Sambamba na hilo Kaimu Mhandisi wa ujenzi Ndg. Bujiku Paul Bujiku alisema changamoto kubwa waliyokutana nayo katika ujenzi huo ni uhaba wa saruji hivyo kupelekea mradi kuchelewa kukamilika kwa wakati kama ilivyokua imetarajiwa awali.
`
Takribani jumla ya shilingi milioni 299 zimetumika kati ya shilingi milioni 440 ambazo zilitolewa kwa lengo la kukamilisaha mradi huo kwa mchanganuo ufuatao, Vyumba 14 vya madarasa Tsh 280 Milioni, Jengo la Utawala moja 30Mil. Nyumba ya mwalimu mbili kwa moja 50Mil, Matundu23 ya vyoo vya wanafunzi shilingi milioni 25,300,000, madarasa mawil iya shule ya msingi mwandege milioni 40, matundu manne (4) ya vyoo vya walimu 1,100,00Mil na shilingi 10,300,000 kwa ajili ya usimamizi na ufatiliaji, ujenzi wa mradi huo unatarajiwa kukamilika mapema mwisho wa mwezi Novemba mwaka huu.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.