Mratibu Mkoa wa Pwani Bi.Roseline Kimaro amewapongeza (CMC)wajumbe Kamati za Jamii kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuwasimamia wanufaika wa mpango TASAF.
Bi.Roseline Kimaro amewatia moyo kutokana na changamoto mbalimbali wanazopitia kipindi cha malipo na kuwataka kuendelea kusaidia walengwa. Hata hivyo kwa kazi wanayofanya imewasaidia kuaminiwa na Wanajamii na kuweza kupata nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Halmashauri ya Kiijiji.
Nae Bi.Safina Msemo Mratibu TASAF Wilaya ya Mkuranga ameendelea kuwasisitiza kuwasimamia walengwa katika mpango wa kuweka akiba na kukuza uchumi na Kaya kuendelea na shughuli za ujasiliamali kupitia vikundi vyao ili kujikwamua kiuchumi.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255222928730
Simu ya Mkononi: 0634329394
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2026 MkurangaDc. All rights reserved.