Katibu Tawala Wilaya ya Mkuranga Omari Mwanga amekutana na Wachimbaji na Wasafirishaji wa Madini ya mchanga kwa lengo la kujadili mambo mbalimbali yanayohusu madini ya mchanga.
Katika kujadili ndaninkikao Kikao hicho ambacho kimefanyika Tarehe 24 Julai 2024 katika ukumbi wa Flex Garden kulikuwa na wasaa wa kusikiliza na kutatua changamoto baina ya Wachimbaji wa Madininhayo ya Mchanga na Wasafirishaji (Madereva)
Mwanga akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Khadija Nassir Ali amewataka wafanyabiashara hao kuweka muafaka wa pamoja ili kuwe na maelewano kwa kuwa wote kwa pamoja wanategemeana katika kutafuta riziki na kulinda maslahi ya biashara zao.
Aidha amesema jukumu la Wilaya ni Ulinza na usalama wa rai na mali zao hivyo ikitokea jambo lolote la uvunjifu wa amani Serikali itasimamia na kuhakikisha usalama unapatikana kwani hii ni biashara huru hivyo ametaka kila mmoja akubaliane kwa jinsi ambavyo kwa kila mtu atakwenda kunufaika.
Kikao hicho kimehudhuriwa na wataalam kutoka Tume ya madini Kanda ya dar es salaam na Pwani, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga na Wataalam wake.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.