Mamlaka ya maji safi na maji taka (DAWASA) wamezindua mradi mkubwa wa maji kwenye Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani ambao utawanufaisha wananchi elfu 25 katika vijiji mbalimbali
Akizungumza katika hafla maalumu iliyofanyika juzi kwenye viwanja vya Halmashauri ya Wilaya Afisa Mtendaji Mkuu wa (DAWASA) Mhandisi CYPRIAN LUHEMEJA alisema huo ni muendelezo wa kisima walichochimba eneo la kurungu mwaka 2015
Uhemeja aliyewakilishwa na msimamizi wa miradi Mhandisi John Kirecha aliweka bayana mradi huo utaogharimu sh bilioni 5.5 kupitia mapato ya ndani utajumuisha ujenzi wa tanki lenye ujazo wa lita milioni 1.5 tenki la kupokea na kusambaza maji hadi kwenye tanki sambamba na ulazaji mambomba urefu wa kilomita (63)
Mhandisi Mrema alitaja maeneo yatakayonufaika kuwa ni pamoja na Mkuranga A,B,Kiguza,Bigwa,sambamba na Mkwalia Kitumbo,Njia Nne, Hoyoyo.
Kwa upande Mbunge wa jimbo la Mkuranga ambaye pia Naibu Waziri wa mifugoAbdalla Ulega alimpongeza Raisi Dk. John Magufuli kwa mikakati yake ya kusimami Mapato ya ndani hali iliyofanikisha Wilaya hiyo iiyofanikisha Wilaya hiyo kupata miradi ya maji na barabara ya jamii kwenda kisiju kama ilani ya uchaguzi (CCM) inayoainisha
Ulega pamoja na kuwapongeza(DAWASA) kwa kuchangia sekta ya Elimu ya afya maalumu mradi huo uwafikie pia wakazi jirani na Mwanambaya, Tengelea,Mbezi Gongoni na Kiparan’ganda huku akisisitiza kipaumbele cha vibarua na wataalam kiwe wenyeji wa wilaya hiyo
Mradi huo unaolenga kumtua ndoo mwanamke sambamba na kuboresha afya za wananchi itahusisha pia ujenzi wa visima kwenye kitongoji cha mpera kijiji cha kisemvule
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.