Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani Khadija Nasri Ali amewaagiza Watendaji kata wote (25) kuhakikisha wanaunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuboresha Sektq ya Eliku kwa kuhakikisha wanahamasisja wazazi na walezi vijiji vyote (125) wachangie chakula mashuleni.
Akifingua kikao cha kawaida cha lishe bora kwa robo ya pili mwaka 2021/22 katibu Tawala wa Wilaya Veronica Kinyemi aliyemuwakilisha kiongozi huyo aliweka bayana mamilioni ya fedha za ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya uviko (19) ambao ni mkopo wa riba nafuu Trioni 1.3 tokq shiroka la fedha duniani (IMF) zimeboresha sekta ya elimu Wilayani humi kufiayia ujenzi wa madarasa (116) kwenye shule za sekondari.
Aidha kiongozi huyo aliweka bayana suqla la lishe bora ni mkakati wa serikali uliozinduliwa na waziri Mkuu Kassim Majaliwa hivyo watendaji kata ndio wasimamizi wakuu katika kufanikisha utekelezaji wa mpango huo ambao utapunguza utoro sambamba na utapiamlo.
Alimalizia kwa kumpongeza Mkurugenzi kwa kununua pikipiki (25) za watendaji kata ambazo zitarahisisha utendaji.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mwantumu Mgonja amewataka watendaji kata wawajibike jwenye vijiji vyao kwa kusimamia huduma bora sekta ya elimu na afya baadala ya kufanya jazi kwa nazoea huku akiahidi kufanya ziara za kushtukiza maeneo mbalimbali na kuchukua hatua za kinidhamukwa wataozembea.
Naye mratibu wa Lishe Mkoani Pwani Pamera Meena aliwasilisha mada mbali mbali zinazolenga kupunguza changamoto za upatikanaji wa lishe bora.
Akiwasilisha taarifa upande wa Halmashauri ya Wilaya Mratibu wa lishe ngazi Vumilia Ngangando alisema mikakati ya kuchangisha chakula mashuleni ulikumbana na changamoto kufuatia matamko ya serikali. Aliweka bayana kutopata chakula wanafunzi kumechangia matokeo ya Mtihani wa Taifa kutopata daraja la kwanza huku akitilea mfano shule ya msingi kiguza kuingia kumi bora ya ufaulu kufuatia wazazi kujamasishana na kuchangia chakula shuleni.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.