Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Bi. Khadija Nasr Ali jana amefanya ziara ya kukagua Ujenzi wa Miradi ya Madarasa mapya ya Sekondari ili kujionea muendelezo wa ujenzi huo sambamba na changamoto zilizopo ili kuzipatia ufumbuzi mapema na hatimae Madarasa hayo yaweze kukamilika kwa wakati na kuweza kupokea wanafunzi wapya wa kidato cha kwanza Mwakani.
Bi Khadija akiambatana na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bi. Mwantum Mgonja sambamba na Kamati ya Ulinzi na Usalama na Wataalam wa Wilaya hiyo walipata fursa ya kufika katika Kata ya Vikindu, mwandege, Kimanzichana na Lukanga na kuona hali halisi ya ujenzi huo ikiendelea vizuri na kwa ushirikiano mkubwa.
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya ameziagiza kamati zote zinazosimamia ujenzi wa Madarasa hayo kuwa makini na kuwataka kusimamia ujenzi huo ufanyike kwa ubora unaotakiwa sambamba na vifaa vya ujenzi kufikishwa katika eneo la ujenzi kwa wakati.
Awali akiwa katika Kata ya Vikindu Mkuu wa Wilaya amewataka Viongozi wa Kata hiyo kuwatumia wadau wa maendeleo walipo ndani ya kata hiyo ili na wao waweze kuchangia katika Miradi hiyo ili kujenga mahusiano mema na kuongeza nguvu ya maendeleo katika Kata hiyo.
Sambamba na hayo wananchi wote ambao wamebahatika kupatiwa Miradi hiyo katika maeneo yao wanatakiwa kushiriki kikamilifu kujitolea nguvu zao katika ujenzi ili kuongeza nguvu na kupunguza baadhi ya gharama ambazo hazina tija katika Miradi hiyo.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.