Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani Khadija Nassir Ali amefungua mafunzo ya Jeshi la Akiba Katika Kijiji cha Kibuyuni Kata ya Panzuo
Akiongea na Askari hao amesema sio kila Mtanzania atakuwa na nafasi ya kujiunga na mafunzo hayo, hivyo amewataka kufahamu kuwa wao ni wateule kwa kuonesha nia na uzalendo na kuwaahidi kuwasimamia na kuhakikisha vijana hao wanakwenda kukamilisha mafunzo hayo.
Amesema mafunzo ya Jeshi la hilo ni mafunzo ambayo yamejawa na tunu pamoja na furaha yenye maono makubwa ambayo yatawafanya vijana mbalimbali nchini kwenda kusimama imara.
"Rais wetu na Amiri Jeshi Mkuu Dkt.Samia Suluhu Hassan amekuwa akihimiza na kuelekeza usimamizi mzuri wa uwendeshaji wa mafunzo haya na mm pia kama Kamanda wenu wa Wilaya nimekuwa nikisisitiza namna nzuri ya kuendeleza usimamizi mzuri wa mafunzo haya ili yaweze kuwa na tija."alisistiza
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255222928730
Simu ya Mkononi: 0634329394
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2026 MkurangaDc. All rights reserved.