Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Khadija Nassir Ali amekemea utaratibu unaotumiwa na waendesha Bodaboda na Bajaji kwa kubeba abiria zaidi ya idadi inayotakiwa.
Kauli hiyo ameitoa leo akiwa anafanya mkutano na waendesha Bodaboda hao katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Wilaya huyo na kuwasisitiza kuacha mara moja kufanya hivyo na wakiendelea serikali nayo itaendelea kuwakamata na kuwachukulia hatua.
Amewataka kushirikiana na kutoa taarifa za kiharifu kwa vyombo vya usalama hasa kwa wale wanaofanya shughuli za usafirishaji nyakati za usiku na kuzitambulisha kazi wanazofanya ili kuhalalisha kazi hiyo ya kusafirisha abiria usiku.
Aidha amewataka kuacha kutumia Pikipiki kwa matumizi ya kubebea Mkaa na badala yake amewataka kushirikiana na serikali kwa kuomba vibali kwa ushirikiano wao ili kuweza kubeba mikaa hiyo kwa vyombo halisi vilivyoruhusiwa kufanya kazi hizo badala ya Bodaboda.
Pamoja na hayo Mkuu wa Wilaya amewataka kujiunga pamoja na kuona ni namna gani wanaweza kupata mikopo ya Pikipiki na kuzimiliki badala ya kuwa watumwa kwa kuingia mikataba na makampuni au watu binafsi na kupelekea kukimbia hovyo barababani kwa lengo la kutimiza malipo ya wamiliki wa vyombo hivyo, na serikali ngazi ya Wilaya iko tayari kushirikiana nao ili waweze kupata Pikipiki hizo.
Madereva hao wa Bodaboda wamemuomba Mkuu wa Wilaya kuwahimiza watu wa usalama kutumia ustaarabu kuwakamata Bodaboda wanapotaka kukagua makosa na mwisho kuharakishiwa kupata leseni zao kwa wale waliopata mafunzo.
Mkuu wa Wilaya ameendelea kufanya mikutano ya makundi mbalimbali ya wananchi kwa lengo la kutekeleza agizo la Mhe. Raisi Dkt. Samia Suluhu Hassan la kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.