Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe.Khadija Nassir Ali Julai 16,2024 amefanya kikao na Watendaji wa Kata na Vijiji katika Ukumbi wa Mwinyi Sekondari.
Amesema Lengo la kikao hicho ni kujipanga kwa ajili ya Mwaka mpya wa fedha na kutakiwa kujua nafasi za kila mmoja pamoja na kuhakikisha anatimiza majukumu na Wajibu wake.
"Nitumie fursa hii kwa uzito wa kipekee kuwapongeza kwa jitihada zenu zilizozaa matunda na hatimae tumefunga mwaka wa fedha 2023-2024 kibabe, alisema Mkuu wa Wilaya
Pia amesema pamoja na wengine kupitia nafasi zao imetuwezesha kufikia malengo ya makusanyo ya mapato ya Halmashauri licha ya changamoto mbalimbali ambazo zimejitokeza."
Amewataka kila mmoja afahamu mazingira na jamii inayomzunguka ili kuongoza katika namna ambayo itamuwezesha uongozi wake kuweza kuonekana na kuacha alama
Aidha amewataka Watendaji kuhakikisha wanafanya mikutano ya vijiji kwa mujibu wa sheria na kanuni kwani wananchi wanatakiwa kujua taarifa za Maendeleo za vijiji vyao na kuwasilisha mihutasari hiyo katika ofisi husika.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255222928730
Simu ya Mkononi: 0634329394
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2026 MkurangaDc. All rights reserved.