Minde Honorata.
June 5, 2021
PWANI
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga amepiga marufuku ukataji miti ya miembe pamoja na kuzuia utolewaji Vibali vya Ukataji wa Miti hiyo, ambayo kwa sasa imeonekana ipo kwenye hatari kubwa ya kutoweka kutokana na kuvunwa kwa wingi kwa ajili ya kuchoma Mkaa
Filberto alitoa maagizo hayo kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira Dunia ambayo Wilayani Mkuranga yaliadhimishwa kwa shughuli za kufanya usafi katika Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga
Alisema tatizo la ukataji miti hususani ya miembe kwa ajili ya kuchoma Mkaa limethiriwa kwa kiasi Kikubwa Wilayani Mkuranga na hivyo amewaagiza watendaji katika idara zote zinazohusika kuhakikisha vitendo hivyo vya ukataji mito ovyo vinadhibitiwa
“miti ya matunda hususani ya miembe inakatwa sana kwa ajili ya kuchoma Mkaa na hali itatupeleka mahali ambapo tunda la embe hatutaliona kwa kuwa miti yake inakatakwa ,hivyo waataam simamieni hili na msitoe vibali vya kukata miti hiyo ili kuepukane na hatari ya kutoweka miti hiyo” Sanga alisema
Kaimu DED Halmashauri ya Mkuranga Benjamini Majoe alieleza shughuli za binadamu kama vile utunzaji mbovu wa ardhi ,matumizi ya endelevu ya rasilimali pasipo kuzingatia utunzaji wa uhifadhi, kilimo cha kando ya vyanzo vya maji ni baadhi ya sababu zinazochangia uhalibifu wa mazingira
“kuna madhara mengi ambayo yanasababishwa na uhalibifu wa mazingira ikiwa ni pamoja na kutoweka kwa makazi ya viumbe hai ,kutoweka kwa baoanuai ,upotevu kwa rasimali za misitu ambazo usababisha mabadiliko ya tabia nchi na uharibifu wa ardhi unaochochea kupunguza uwezo wa udongo katika kuzalisha mazao ya chakula na biashara,” alisema
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mohamed Mwela amewataka vijana kuunga mkono jitihada za serikali za kudhibiti uhalibifu wa mazingira kwa kuanzisha vikundi kupitia mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na halmashauri iili waweze kukusanya taka ngumu na kuziuza kwenye viwanda vya mkoani Pwani
Beatrice Mkera Kaimu Afisa Mazingira Halmashauri ya Mkuranga amezungumzia vitendo vya ukataji miti ovyo katika makazi ya Wanyama kunavyosababisha baadhi ya Wanyama wakali kuonekana kwenye maeneo ya makazi ya watu kwa kuwa maeneo yao ya asili yameathiriwa”
‘sasa hivi tunaona Wanyama kama tembo , simba wanaonekana katika maeneo ya makazi ya watu na haya yote ni matokeo ya watu kuvamia kwenye makazi ya Wanyama hao na kukata miti kwa ajiil ya kuchoma mkaa na si Wanyama wakubwa pekee wanaoathirika bali hata bakteria wa kuzalisha udongo wapo hatarini kupotea ’ Beatrice alisema
Kauli mbiu ya Mwaka huu ya maadhimisho ya siku ya mazingira duniani ni matumizi ya nishati mbadala kuongeo mfumo wa Ikolojia
MWISHO
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.