Mkuu wa Wilaya ya mkuranga Mkoa wa Pwani Filberto Sanga amewapongeza walimu wa shule za sekondari kwa kuandaa wanafunzi katika mazingira mazuri hali iliyochangia kupandisha ufaulu kwenye Mkoa na Taifa kwa ujumla.
Akizungumza kwenye hafla ya tathminikwa wahitimu kidato cha pili ,nne na sita iliyofanyika sekondari ya Ujenzi iliyopo Mkuranga leo 16/3/2021.
Sanga aliyewakilishwa na Afisa Tarafa Kisiju Kenedy Isararaaliwataka Madiwani, Watendaji Vijiji na Kata kutumia vikao vyao vya kisheria kuhamasisha wazazi walezi sambamba na wadau wa maendeleo kuchangia chakula hali itakayoongeza ufaulu.
Kwa upande wake Afisa elimu Sekondari Benjamini Majoya aliweka Bayana uwajibikaji wao bila kuzingatia changamoto wanalenga kutekeleza sera ya elimu mwaka 2014, elimu bilamalipo ilani ya uchaguzi mwaka 2020-25na hotuba ya Rais Dkt JohnMagufuli wakati alipozindua Bunge.
Katika hafla hiyo shule mbali mbali zilizofanya vema, walimu na wanafunzi kwnye mitihani ya kidato cha pili ,nne na sita walitunukiwa vyetina pesa huku sekondari binafsi centennial Christian seminari ikiibuka mshindi maeneo yote,mwinyi ikiongoza matokeo kidato cha sita , mamdimkongokidato cha nne.
Akifunga hafla hiyoMwenyekitiwa kamati ya kudumu Huduma za jamii Hassani Dunda aliweka wazi kuwa kwa sasa wana mahitaji makubwa ya walimu na taarifa zinaenda sana Serikali kuu kuwasilisha mahitaji yao kama Wilaya ya kuongezewa walimu.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.