Wananchi wa Kata ya Mkuranga wamempongeza Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Khadija Nassir Ali kwa utendaji wake mzuri wa majukumu yake ambayo yamechochea kuleta maendeleo ndani ya Wilaya ya Mkuranga.
Pongezi hizo zimetole na wananchi hao katika Mkutano wa hadhara uliofanyika tarehe 26 Septemba 2024 kwenye viwanja vya stendi kuu ya Mkuranga.
Akihutubia katika Mkutano huo Mkuu wa Wilaya amewataka watumishi wote kuwapa kipaumbele wazee pale wanapokuja kupata huduma mbalimbali katika ofisi na kuwathamini na kuwajali kwani wazee ni tunu ya Taifa.
Amesema Halmashauri imetenga Bajeti ya kiasi cha shilingi Mil 50 kwa ajili ya kununua mafuta yatakayotumika kwenye Greda ambalo litakalotumika kusafisha barabara za mitaa katika Kata mbalimbali ambapo tayari kazi hiyo imeshaanza ili kurahisisha huduma bora za usafiri kwa Wananchi.
"Barabara ya Tengelea imepata fedha ya kuchongwa km 6 na Tarura imetenga Bajeti ya kiasi cha shilingi 110,300,000 kwa ujenzi wa box culvert ambalo limeharibika kutokana na mvua zilizonyesha hivi karibuni na Mkandarasi yupo ambapo kwa sasa anamalizia majukumu ya ujenzi wa miundombinu mingine ndani ya Halmashaur" ( alisisitiza ).
Aungumzia uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mkuu wa Wilaya amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika daftari la kudumu la wapiga kura kuanzia October 11-20,2024 na kuwataka Wananchi wenye sifa hasa Vijana kujitokeza kwa wingi katika kugombea nafasi za uongozi kwani uchaguzi huu ni huru na haki ya kila mwananchi.
Mpaka sasa ametembelea Kata 23 kati ya Kata 25 na kukagua miradi ya maendeleo 108 ikiwa ni Maelekezo mahsusi ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kuwataka wakuu wa Wilaya kushuka chini kuchukua maoni,kusikiliza na kutatua kero za wananchi sambamba na kukagua miradi ya maendeleo ili kuhakikisha thamani ya fedha inaendana na kazi inayofanyika.
Pia amekagua miradi ya maendeleo Kata ya Mkuranga katika Kijiji cha Mkwalia, Sunguvuni,Mgawa na Mwasani huku akiwa ameongozana na Kamati ya Usalama ya Wilaya,Kaimu Katibu Tawala,Kaimu Mkurugenzi na Wataalamu wake na Wakuu wa Taasisi Wezeshi.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.