Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani Khadija Nasri amewataka Madiwani wajikite zaidi katika kuwaletea maendeleo wananchi .
Akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani robo ya nne April hadi Juni mwaka 2020-21 kiongozi huyo ambaye ni kikao chake cha kwanza aliwataka wawakilishi hao wa wananchi wasimamie ipasavyo vyanzo vya mapato sambamba na kuelimisha wananchi walipe kodi.
Aidha Khadija aliweka bayana mafunzo ya kusimamia na kuibua mapato watakayopata wataalam wa Halmashauri hii katika mpango wa Taifa kwa Halmashauri (27) anaamini yataleta mageuzi na kupaisha mapato yatakayofanikisha kuboresha miradi ya maendeleo.
Akizungumzia Idara ya kilimo aliwataka wajikite katika kuzalisha malighafi ambazo zitatumika kwenye viwanda vya ndani ya Wilaya hali itakayochangia kuboresha maendeleo ya wakulima
Kwa upande wake Mkuu huyo wa kamati ya ulinzi na usalama aliwatoa hofu wananchi kuwa taarifa za uwepo wa simba kwenye msitu wa hifadhi ya vikindu ni uzushi huku akitangaza uwepo wa tamasha kubwa la utalii mwezi oktoba tarehe 2 ambapo itaongozwa na Waziri wa maliasili na utalii.
Diwani wa Kata ya Mipeko Adili Kinyenga alilitaka baraza kuwa na mpango Madhubuti sambamba na kutunga sheria ndogo ili kupanua wigo wa kukusanya mapato kwenye madini ya mchanga ikiwemo kununua mizani za kupima kila lori la mchanga badala ya shilingi elfu (20) ya sasa.
Katibu Tawala Wilaya Veronica Kinyemi alipongeza jitihada za Madiwani wakishirikiana na Wataalam kufanikisha ukusanyaji mapato ya ndani sambamba na hati safi miaka mitatu mfululizo.l
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mohamedi Mwela alifunga kikao aliomba mshikamano kwenye ukusanyaji mwaka 2022-23 na kuahidi kuvalia njuga chanzo kiku cha mapato kwenye utalii na kuhimiza maboresho Mkuranga yalingane na makusanyo.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.