Wakazi wa wilaya ya Mkuranga wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuhudhuria Clinic ya macho itakayoendeshwa kwa muda wa wiki mbili katika hospitali ya wilaya ya Mkuranga (Mkwalia)
Wito huo umetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe Filberto Sanga pamoja na Meneja Mkuu wa Shirika la Rehema Foundation Bw. Zuberi Said Salum hospitalini hapo katika ufunguzi wa Huduma ya upasuaji wa mtoto wa jicho itakayoendeshwa hospitalini hapo kwa muda wa wiki mbili kuanzia leo kwa udhamini wa shirika la Deniz Feneri la nchini Uturuki.
Sanga alisema, kama serikali wameipokea huduma hiyo kwa mikono miwili kwani itakua na msaada mkubwa kwa wananchi wa wilaya hiyo wasioweza kumudu gharama za matibabu kwani huduma hiyo itatolewa bure kabisa, hivyo kuwataka wananchi kuhudhuria kwa wingi ili kupata huduma hiyo ndani ya wilaya yao.
Amesema wilaya ina changamoto nyingi katika sekta ya Afya lakini hili ya upasuajiwa macho lilikua halina mbadala kwani kwa magonjwa mengine msaada ulishapatikana kwa kiwango chake.
Pia alilishukuru shirika la Rehema Foundation kwa kuichagua wilaya ya mkuranga kuwa miongoni mwa wilaya zitakazonufaika na huduma hiyo kwani wilaya nyingi zilipeleka maombi,na kuwa kiunganishi kikubwa na shirika hilo la Deniz Feneri kutoka uturuki maana imekua msaada mkubwa kupunguza tatizo la macho kwa wakazi hao au kulimaliza kabisa.
Kwa upande wake Bwana Salum ambaye ni meneja washirika la Rehema Foundation mbali na kuishukuru Serikali ya Tanzania kupitia Mkuu wa wilaya ya Mkuranga na shirika la Deniz Fenerila nchini Uturuki ambalo Duniani linafanya shughuli zake katika nchi16 ,alisema mradi huo wa upasuaji wa mtoto wa jicho unalengo la kuwasaidia wananchi ambao wana uono hafifu kutokana na matatizo hayo, ‘lengo ni kuwafanya wananchi waweze kupata uono bora na kuendelea na ujenzi wa taifa kama kawaida’ .
Aidha wananchi waliohudhuria zoezi hilo walipongeza jitihada hizo za serikali na mashirika hayo kwa ujumla kwani watu wengi hushindwa kupata huduma stahiki kutokana na gharama za matibabu na umbali kwani huduma nyingi hutolewa katika hospitali yaTaifa Muhimbili.
“Tunashukuru kwa huduma hii kuletewa hapa karibu mana wengine inatuwia vigumu kwenda mpaka Dar es Saalam”
Ufunguzi huo pia ulihudhuriwa na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Bi. Yassemin Eralp, ambapo mbali na huduma hiyo pia walitoa msaada wa nguo na viatu vya watoto katika wodi ya watoto hospitalini hapo.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.