Mkuu wa wilaya ya mkuranga Mh. Filberto Sanga amepongeza jitihada zinazofanywa na jukwaa la wadau wakilimo (ANSAF) katika kuboresha afya na kipato cha wakazi wa wilaya hiyo
Sanga alisema hayo jana wakati wakufunga rasmi awamu ya nne ya Mradi wa kusambaza mbegu bora za viazi lishe ‘Sambaza Mbegu Fasta’ (Fast Trade Project) ulio chini ya wizara ya kilimo Tanzania na Zanzibar na ufadhili wa mfuko wa Bill & Melinda Gates wa nchini Marekani.
Amesema anafurahishwa na nguvu iliyowekwa na shirika hilo katika kutoa elimu ya lishe kwa wananchi, kusambaza mbegu na kusimamia vyema shughuli za kilimo na pia utengenezwaji wa bidhaa mbalimbali zinazotokana na zao la viazi lishe.
Sanga pia aliwapongeza wananchi waliotumia fursa hiyo kujitengenezea kipato baada ya kusambaza mbegu za viazi nakuuza mazao ya viazi na bidhaa mbalimabali zitokanazo na zao hilo kama vile, unga wa lishe, tambi, keki, chapati, ‘juice’ ya viza lish na kadhalika pamoja na kuimarisha afya za familia zao.
Sanga alisema, anapendendekeza lishe hiyo ianze kutolewa katika shule za sekondari pia ilikuboresha afya za wanafunzi hao itakayopelekea kuboreka matokeo kitaaluma kwani wanafunzi wakiwa na uhakika wakupata chakula shuleni, itaboresha mahudhurio yao lakini pia Vitamin A inayopatikana kwa wingi katika zao hilo ni muhimu katika kuimarisha afya na akili pia.
Aliongeza kuwa imefika wakati kwa wanainchi hao kuunga mkono jitihada hizo kwa vitendo ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa watu wengine bila kusubiri vikao vya wataalamu hao kutoka ANSAF bali wale waliopata elimu hiyo awali watumike kuisambaza kwa watu wengine ili kuleta matokeo bora zaidi.
Naye Mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa miwa – Kibaha (Sugarcane Research Institute - Kibaha) Dr. Kiddo Mtunda akielezea mafanikio ya mradi huo unaoshirikiana na vituo vya utafiti wa kilimo Mikocheni, Kizimbani na KOLPING, alisema viazi lishe ni zao muhimu kwaTanzania na linashika nafasi ya pili likitanguliwa na zao la mihogo katika mazao ya mizizi. Na kama likilimwa vema linaweza kutokomeza kabisa tatizo la uhaba wa chakula na lishe bora katika familia.
Dr. Kiddo alisema katika mradi huo wa ‘Sambaza mbegu fasta’ kinachofanyika ni kugawa mbegu katika wilaya hiyo kwa kutumia wanafunzi wa shule za msingi kwa kuchagua wanafunzi 200 wanaotoka kaya tofauti, “Tunawapa mbegu 120 kila mmoja zikiwa kwenye makundi manne tofauti, kisha kuwaagiza wanafunzi hao kuwapa wazazi wao ambao nao hupata mafunzo ya kuzipanda”
Alisema kwa asili wakulima walizoea kulima viazi vitamu vyenye rangi nyeupe au ya maziwa kwa ndani lakini kuna viazi vyenye rangi ya karoti kwa ndania mbavyo vina vitamini A kwa wingi. Kutokana na kuwa na vitamiani A kwa wingi ni faida kwa afya ya macho, ngozi, ukuaji bora na pia huimarisha kinga ya miili yetu dhidi ya maradhi, “vitamin A zenye karotini husaidia sana kusafisha mwili na kutukinga dhidi ya maradhi na kuzeeka kabla ya wakati wetu”,
mbali na utaratibu wa kuhamasisha uzalishaji wa mbegu bora na safi za viazi lishe kwa kuwatumia wanafunzi wa shule za msingi kufikisha mbegu hizo katika familia zao, lakini pia kutakua na uelimishaji wa wanafunzi hao kupitia vibonzo/katuni ziyakazoandaliwa na msanii Masoud Kipanya kwa kuaandaa vitabu vitakavyosambazwa shuleni.
Akizungumzia ufanisi wa mradi huo huku akimtolea mfano mkulima Festus Sebastian Dr. Kiddo anasema zao hilo likizalishwa kwa njia bora sio tu husaidia kupata chakula cha uhakiaka bali ni fursa nzuri kibiashara kwa ziada inayobaki kwani gunia moja la viazi lishe linauzwa kwa Tsh30000 hadi Tsh40000.
Lengo hili litasaidia kupunguza kama si kumaliza kabisa matatizo ya uhaba wa chakula na kushambuliwa na maradhi.
Naye mtaalamu wa lishe kutoka chuo cha utafiti wa kilimo Mikocheni (MARI) Bi. Domina Nkuba, alielezea umuhimu wa lishe hiyo kwa watoto, wanawake wajawazito na wanaonyonyesha pamoja na wanaume na kutoa takwimu za mafanikio “mpaka sasa tumeshatoa elimu kwa wakulima 624 kati yao wanawake ni 277 ndani ya wilaya ya mkuranga lakini elimu hiyo pia ilitolewa kwa maafisa Afya, walimu na maafisa lishe”
Wakati huohuo alikabidhi nakala za vitabu 1200 kwa mgeni rasmi wa mkuu wa wilaya kwaajili ya kuvisambaza katika shule za ndani ya wilaya hiyo ikiwa ni mpango wakueneza elimu zaidi juu ya faida ya zao la viazi lishe na pia kuwaelimisha wananchi juu ya mgawanyiko sahihi wa makundi ya vyakula kwani kumekua na uelewa tofauti katika jamii juu ya makundi hayo.
Alisema uelewa juu ya elimu ya lishe na matumizi sahihi umeendelea kuongezeka siku hadi siku toka asilimia 50 mwanzo wa mwaka 2015 hadi asilimia97 mwaka huu.
Naye Afisa elimu wilaya ya Mkuranga Ndg. Cosmas Magige akichangia katika mkutano huo alipendekeza kufanyike jitahada za kuwapikia wanafunzi lishe hiyo shuleni ili kuimarisha afya zao na kupunguza utoro shuleni.
Kwa upande wake Afisa lishe wilaya Bi. Vumilia alisisitiza matumizi ya viazi lishe kwa wakazi wa wilaya hiyo ikiwa ni mpango wakupunguza tatizo la upungufu wa damu kwa wagonjwa wanaohudhuria tiba katika zahanati mbalimbali kwani takwimu zinaonesha asilimia 70 ya watu wanaopimwa hukutwana upungufu wa damu hivyo msisitizo katika ulaji wa viazi lishe pamoja na majani yake itakua suluhu ya tatizo hilo badala ya uchangiaji damu ambao una changamoto nyingi mpaka sasa.
Mwenyekiti wa kamati ya Uchumi wilaya na diwani wa kata ya Tengelea Mh.Shaban Manda alisema wapo tayari kuongeza nguvu katika kuelimisha jamii ili kuunga mkono juhudi za kuimarisha afya na kipato kutokana na zao hilo.
Mmoja ya wakulima waliofanikiwa kulima zao hilo, Festus Sebastian amezungumzia faida aliyoipata kutoka na na zao hilo “viazi lishe vinatoa viazi vingi sana na tangu nimeanza kilimo hiki nimeshagawa mbegu kwa wakulima 20 kama mradi unavyotaka”
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.