Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mh.Filberto Sanga ametoa maagizo makali kwa wananchi na viongozi wanaoshiriki kukata miti hovyo kwa matumizi yao binafsi hasa miti ya miembe na minazi.
Mh Sanga aliyasema hayo hapo jana wakati maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika kiwilaya kwenye kijiji cha Mwarusembe wilayani Mkuranga.
Mh Sanga aliongeza ”Nitumie nafasi hii kusema sasa miembe na minazi isikatwe mpaka upate kibali kutoka kwa Ofisa Misitu na ofisi za Wakala wa Misitu na mtu asipofuata utaratibu huo hatua kali zitachukuliwa, kuendelea kukata miti hiyo itasababisha kukosa embe na nazi za kutosha katika wilaya yetu"
Mh Sanga aliendelea kusema kwamba iwapo ikionekana gari limebeba miti ya miembe au minazi gari hilo litakamatwa na muhusika ataeleza namna alivyopata hiyo miti na watu wote waliohusika na upatikanaji wa miti hiyo watachukuliwa hatua za kisheria.
Pamoja na mambo mengine Mh Sanga alisema kupitia Muungano wetu ulioasisi taifa hili Serikali ya awamu tano chini ya uongozi shupavu na madhubuti wa Mh.Rais Dkt. John Pombe Magufuli imeweza kuonyesha mafanikio mengi katika Nyanja za ulinzi na usimamizi bora wa rasilimali za taifa, kuimarisha nidhamu ya kiutendaji ndani na nje ya taasisi za umma,kupambana kikamilifu na ufisadi, rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mhandisi Mshamu Munde alisema Muungano unasisitiza mambo mengi ya maendeleo ikiwemo uwezeshaji wa vikundi vya wanawake,vijana na walemavu.
Mhandisi Mshamu aliongeza kwamba Miaka 54 ya Muungano iwe chachu ya kujiunga kwenye vikundi ili kufanya shughuli za maendeleo kwani Halmashauri inakopesha kwenye vikundi badala ya mtu mmoja mmoja.
Bi Faiza juma mkazi wa Mwarusembe alisema miaka 54 ya Muungano katika Wilaya ya Mkuranga kumekuwa na ongezeko kubwa za zahanati na vituo vya afya na kati ya hizo zilizo nyingi zinatoa huduma hivyo kurahisisha utoaji wa huduma za kiafya kwa wananchi.
Muungano umekuwa na faida nyingi sana kwa taifa na watu wake.Miongoni mwa faida hizo ni amani na utulivu, uzalendo na mshikamano, udugu, upendo na urafiki, itifaki na utangamano wa kiuchumi na diplomasia ya kitaifa na kimataifa.
Faida hizi zimekuwa ni msingi imara wa maendeleo yetu kwa vizazi vyote hivyo basi hatuna budi kuudumisha Muungano wetu ili tuendelee kufaidi matunda ya
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.