Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Waziri Kombo amefanya kikao kazi na Maafisa Afya wa Kata 25 zilizopo ndani ya Wilaya ya Mkuranga.
Kikao hicho kimefanyika Tarehe 24 Julai 2024 katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri kikiwa na l3ngo la kukumbushana wajibu na majukumu ya kazi zao.
Kombo amewataka Maafisa Afya hao kufuata sheria, kanuni na taratibu za afya zilizopo sambamba na kutoa elimu kwa jamii ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko.
Aidha amewataka kutumia (Pos) mashine ya kukusanya mapato kwa ajili ya faini ili fedha wanazokusanya zionekane katika mapato ya Halmashauri ambao wanatakiwa kukusanya kwa 10%
Nae Afisa Utumishi Patrick saduka amewataka kufata utaratibu wa utozaji wa faini ili kupunguza malamiko kwa wananchi.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.