Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mwantum Mgonja leo amefanya ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa Madarasa mapya ya Sekondari katika kata 3 miongoni mwa kata 25 zilizobahatika kupata madarasa hayo.
Mwantum akiongozana na Wakuu wa Idara na Vitengo ametembelea Madarasa hayo yanayojengwa kupitia fedha kutoka serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mh. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Ziara hiyo imefanyika kwa lengo la kuhimiza na kufanikisha kumalizika kwa Miradi kwa wakati ili kuweza kuyakabidhi Madarasa hayo kwa Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga mapema wiki hii.
Aidha Mwantum akiwa katika kikao cha Majumuisho ya ziara hiyo amemtaka Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari Benjamin Mayoya kuchukua hatua kwa Wakuu wote wa Shule zenye Mradi ambao watasababisha na kukwamisha ujenzi wa madarasa hayo
Wilaya ya Mkuranga inaendelea kutekeleza na kukamilisha ujenzi wa Madarsa 132 baada ya kupokea fedha kiasi cha Bilioni 2.64.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.