Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Waziri Kombo amefanya ziara ya kukagua Miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuona kasi ya mwendelezo wa ujenzi wa miradi hiyo.
Katika ziara hiyo Mkurugenzi aliongozana na wakuu wa Idara na vitengo na kufanikiwa kukagua miradi ya Afya, Elimu, miundo mbinu ya barabara pamoja na shughuli mbalimbali zinazofanywa na baadhi ya wawekezaji wa viwanda.
Akiwa katika Shule ya Sekondari Kilimahewa iliyopo Kata ya Kimanzichana Kombo amekuwa mkali kwa wazabuni wanaopewa miradi hiyo kwa kushindwa kukamilisha ujenzi kwa wakati.
Aidha amewataka wakuu wa Idara husika pamoja na Mhandisi wa ujenzi kusimamia miradi hiyo kwa ukaribu ili kujua changamoto zilizopo na kuzipatia ufumbuzi mapema na hatimae miradi hiyo ikamilike kwa kiwango stahiki na kwa wakati.
Nae Diwani wa Kata hiyo Yahaya Mnyengema kwa niaba ya wananchi wa Kimanzichana ametoa shukrani kwa Serikali kwa kupeleka fedha za miradi vijijini kwa wakati na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kuihamasisha jamii kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Ziara hiyo ilikuwa na lengo la kuona miradi iliyopelekewa fedha inakamilika kwa wakati na kwa kiwango kinachoendana na thamani ya fedha zilizopelekwa
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.