Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani Filberto Sanga amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mhandisi Mshumu Munde na Wataalamu wake kwa kufanikisha Uchaguzi Mkuu uliopita kuwa wa haki hali iliyofanikisha utulivu na amani.
Akifungua kikao cha Baraza la Ushauri Wilaya ya Mkuranga leo, sanga ambaye ni Mwenyekiti wa kikao hicho alisema Wilaya ina mafanikio makubwa kufuatia ushirikiano wa Madiwani, Wataalamu na Ofisi yake hali ilichangia kuwa Wilaya ya Mfano kwenye huduma za jamii na uwekezaji wa Viwanda.
Kiongoozi huyo aliwataka Wajumbe kujipanga upya kutatua changamoto mbalimbali kwenye sekta ya Elimu hususani kutekeleza maagizo ya Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa aliyetaka ifikapo Februari 28 Mwaka ujao wanafunzi wote wawe Darasani huku wakikaa kwenye Madawati.
Akiwazungumzia Wajasiriamali Sanga, aliwaagiza watendaji Kata na Vijiji kuhakikisha wafanyabiashara wote wawe na Vitambulisho, vinginevyo wakiukaji walipie ushuru husika sambamba na watumishi kuwa na kauli nzuri na uadilifu kwenye matumizi ya Pesa za Serikali vinginevyo wasiorejesha watachukuliwa hatua za kisheria.
Pamoja na hayo Mwenyekiti huyo alimtaka Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya Mohamedi Mwela kusimamia mchakato wa uwepo wa Mji Mdogo wa Mkuranga ambao utachangia kupaisha maendeleo ya Wilaya sambamba na kutatua migogoro ya ardhi, Wafugaji na wakulima pia uwepo wa uwanja wa michezo.
Katika baraza hilo taasisi wezeshi TANESCO, TARULA, DAWASA, RUWASA, TFS, NMB na TRA nao walipata fursa ya kushiriki kwa lengo la kuimarisha huduma mbalimbali ndani ya Jamii ya wana Mkuranga.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.