Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Eng. Mshamu Munde amewashauri vijana kuzingatia nidhamu, ushirikiano, kulinda afya zao pamoja na kujali muda ili waweze kufanya vizuri katika michezo
Akizungumza wakati kuwaaga wanafunzi wa shule za Sekondari Wilayani hapa waliochaguliwa kwenda Wilayani Kibiti kushiriki Mashindano ya siku 7 (kuanzia 31/06 hadi 06/06) ya Umoja wa Michezo na Sanaa kwa Shule za Tanzania (UMISSETA)
Mashindano hayo yatashirikisha Halmashauri zote za Mkoa wa Pwani na baadaye wanafunzi watakaofanya vyema kutoka Halmashauri zote wataunda timu ya pamoja ya Mkoa itakayojumuisha jumla ya wanafuzi 100 watakaoenda Mtwara kushiriki Mashindano hayo ngazi ya Taifa yatakayoanza tarehe 07/06 hadi tarehe 21/06
Munde alisisitiza wanafunzi hao kuzingatia nidhamu , ushirikiano na kujali muda ili waweze kuipeperusha vyema wilaya ya Mkuranga na vilevile kwa kufanya kwao vyema ni kujiandalia fursa nyingine ya ajira kwani sasa michezo ni ajira tosha
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga akisisitiza jambo wakati wa kuwaaga wanafunzi wa shule za sekondari watakaoshiriki mashindano ya UMISETA
Aidha, Munde aliwapongera Walimu waliojitolea kuacha kazi zao za msingi na kujikita kuwafundisha Wanafunzi hao bila malipo yoyote ya ziada, na akawataka kuendelea na moyo huo
Kwa upande wake Kaimu Afisa Elimu Sekondari Wilaya Bi. Clea Haule aliwataka vijana hao kuweka juhudi zaidi na kuipeperusha vyema wilaya katika uga wa michezo huku akisisitiza hakuna linaloshindikana kama mtu ukiweka nia katika kufanikiwa
Jumla ya wanafunzi 80 (Wasichana 44 na Wavulana 36) pamoja na walimu wa michezo waliagwa hapo jana katika shule ya sekondari Mwinyi walipokua wameweka kambi na watekwenda Kibiti kushiriki michezo mbalimbali ikiwemo Mpira wa miguu (wavulana na wasichana), Netiboli, Riadha , ‘Handball’ na Fani za ndani (Kwaya na ngoma)
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.