Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga Ndg. Mwantum Mgonja, amewataka Madereva waendeshao Pikipiku ya Miguu miwili (Bodaboda ) katika Stendi ya Daladala Mkuranga kuacha mara moja kukaa na kukimbilia Magari yanayoshusha Abiria.
Ameyasema hayo lipotembelea stendi hiyo jana na kumuagiza Afisa Biashara wa Wilaya kutenga eneo maalum kwa ajili ya Bodaboda ili kuondoa kero zinazojitokeza kwa Abiri awanaotumia stendi hiyo.
Aidha Mwantum amewataBodaboda hao kuunda uongozi utakaoweza kuwatambua kwa idadi yao kamili na kumpatia taarifa hiyo ya idadi yao mapema.
Abiria wengi wanaotumia kituo hiko wamekuwa wakipata changamoto nyingi kutoka kwa Waendesha pikipiki hizo (Bodaboda ).
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.