Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Waziri Kombo amewapongeza watendaji wa vyama vya ushirika na wasimamizi ubora wa zao la Korosho na ufuta kwa jitihada wanazoonyesha katika usimamizi wa mazao hayo.
Pongezi hizo amezitoa leo kwenye ukumbi wa mikutano wa kituo cha upashanaji Habari Kilichopo Mkuranga (Kiguza ) alipokuwa akizungumza na watendaji hao ambao wanapatiwa mafunzo mbalimbali kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa zao la Korosho
Aidha amewataka wawe waadilifu baada ya mafunzo hayo sambamba na kukaa na kujiuliza ni kwanini Mkuranga tunashindwa na wilaya nyingine na kuona kuangalia changamoto na kuzitafutia majibu yatakayoenda kulifanya zao hilo la Korosho kuwa na thamani
Awali akifungua Mafunzo hayo Kombo amewataka watendaji hao kupitia vyama vyao wakishirikiana na wataalamu wa kilimo kuwa wanahakikisha wakulima wanaandaa mashamba yao mapema na kuyasafisha vizuri sambamba na kutumia viwatilifu kwa usahihi
Akimkaribisha Mkurugenzi Mtendaji, Mwenyekiti wa Chama cha ushirika Mkoa wa Pwani Mussa Ngeresa amesema kwamba kwa sasa hakuna kiongozi atakayebaki katika uongozi kama utakuwa umefanya ubadhilifu wa aina yoyote
Amesema kwa msimu wa Mwaka huu 2025 hawatarajii kuona ubadhilifu wa aina yoyote kwani wao kama chama cha ushirika wamejipanga kuhakikisha katika manunuzi ya Korosho za Mwaka huu hakutakuwa na makandokando
Mafunzo hayo yatakayodumu muda wa siku tatu yanaendeshwa na wakufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Ushirika (Moshi) pamoja na Bodi ya Korosho.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.