Katika kuunga mkono sera ya Tanzania ya viwanda na utimizaji wa adma ya serikali ya awamu ya tano kuwa na uchumi wa kati, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Eng. Mshamu Munde amependekeza uanzishwaji wa uwekezaji kwa ubia.
Akiyasema hayo katika kikao cha kamati ya ushauri ya wilaya (DCC), Eng. Munde alisema imefika muda Halmashauri ianze kuwekeza yenyewe ama kwa ubia ambao utaipa Halmashauri ‘share’ / gawio ili hata siku muwekezaji akiamua kuondoka atakiacha kiwanda kikiwa hai.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Mkuranga, Eng. Mshamu Munde, akisisitiza jambo katika kikao cha kamati ya ushauri wa wilaya (DCC) kilichafanyika tarehe 4 Januari katika ukumbi wa 'Resources Centre' - kiguza wilayani hapa, kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Filberto Sanga.
Aliongeza kuwa kwasasa Halmashauri ina viwanda zaidi ya 61 lakini wawekezaji hao wanakuja na agenda zao kibiashara ambazo haziinufaishi zaidi Halmashauri. Alisema serikali inapendekeza Halmashauri zitafute Miradi ya kimkakati kwa kuandaa maandiko ambayo serikali itatoa fedha kufanikisha miradi hiyo na kwa kuanzia Halmashauri ya Mkuranga imepanga kuanza na stendi ya mabasi –Kipala pamoja na soko la samaki –Kisiju
Munde pia aligusia suala la uwajibikaji wa wawekezaji kwa wananchi katika kusaidia miradi ya kijamii na shughuli za maendeleo.
“Viwanda vingi au wawekezaji wengi hii dhana kidogo imekua ngumu kwao, inakua kama wanalazimishwa kumbe ni wajibu wao, wanapofanya uwekezaji sehemu fulani sehemu ya faida yao lazima wairudishe kwa jamii” alisemaa Eng. Mshamu Munde
Kikao hicho kilichokua na lengo la kutoa taarifa mbalimbali za utendaji wa kazi za serikali ndani ya Halmashauri ya Wilaya Mkuranga, kilishirikisha wadau mbalimabalia wakiwamo Madiwani, wakuu wa idara Halmashauri pamoja na wadau wengine
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.