Wakurugenzi wa Halmashauri za Miji, Wilaya na Majiji Kote Nchini wametakiwa kupanga mikakati ya ukusanyaji mapato ya ndani ili yafikie asilimia (50) ya malengo hatimaye wafanikishe azma ya Rais Dkt John Magufuli ya kuwatatulia wananchi changamoto katika Sekta mbalimbali.
Akizungumza na wataalam na Taasisi wezeshi Wilayani Mkuranga jana Naibu Waziri wa Tamisemi ambaye anashughulikia Afya, Miundo mbinu na Mapato Dkt Festo Dugange alimpongeza Mkurugenzi wa Halmashaauri ya Wilaya ya Mkuranga Mhandisi Mshamu Munde kwa kukusanya asilimia (42) hadi Novemba hali inayoashiria kuvuka malengo.
Kiongozi huyo alimwagiza Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Dkt Stephen Mwandambo kusimamia ufungaji mifumo ya (TEHAMA) kwenye Zahanati na vituo vya Afya ili kuboresha mapato ya sekta hiyo sambamba na kuwafuatilia wapokea pesa za mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii iliyoboresha (ICHF) na kuhakikisha zinawekwa kwenye akaunti baada ya kulipwa hatimaye wanufaika wapate kadi sambamba na kuboreshe huduma ya Afya.
Dkt Festo amemwagiza Meneja wa Wakala wa barabara Mijini na Vijijini (TARURA) Mkuranga Mhandisi Godfrey Mlowe kushirikiana na TANROAD kupima uzito wa magari ya mizigo ukiwemo Mchanga yanayopita Vijijini ili yanapoharibu Miundombinu kwa kuzidisha uzito yapigwe faini.
Aidha amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mhandisi Mshamu Munde, kutenga Bajeti kwa ajili ya kuanzisha walau huduma za OPD katika kituo cha Afya kipya kilichopo kijiji cha Vikindu ili wananchi walio karibu na kituo hiko wapate huduma za afya kwa ukaribu huku mchakato wa kuongeza majengo kituoni hapo ukiendelea.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na michezo Abdallah Ulega ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga alisema kupitia Baraza la Madiwani wamejipanga kutenga shilingi Bilioni moja kila Mwaka ili kusaidiana na TARURA kufungua mtandao wa Barabara Vijijini huku akiwataka Wataalamu Sekta ya Afya kuhakikisha wanaimarisha huduma kwa wanufaika wa (ICHF).
Naye Mkuu wa Wilaya Ya Mkuranga Filberto Sanga aliitaka Hospitali ya Wilaya kuondoa changamoto ya wanufaika wa Bima kutopata baadhi ya Dawa hapo huku maduka Binafsi zikiwepo Dawa zote
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.